Ubaguzi wa rangi waripotiwa kukithiri nchini Marekani

Wamarekani weusi wanaamini kuwa hali ya ubaguzi wa rangi nchini humo itazidi kuwa mbaya.

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa kwa pamoja na gazeti la Marekani la Washington Post na taasisi ya uchunguzi wa maoni ya Ipsos yanaonyesha kuwa asilimia 51 ya raia weusi wa Marekani hawana matumaini ya kuboreshwa hali ya ubaguzi wa rangi nchini humo.

Katika utafiti huo, 3% ya watu weusi waliohojiwa wamesema kuwa hali ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani itabaki kama ilivyo. Asilimia 11 kati ya Wamarekani ndio tu walioonyesha matumaini ya kuboreshwa hali hiyo.

Takriban 70% ya washiriki katika utafiti huo, ambao wana umri wa kati ya miaka 50 na 64, wamesema hali ya sasa ya maisha ya barobaro na viijana weusi wa Marekani ni ya hatari zaidi kuliko hapo awali.

Wakati huo huo, 60% ya watu wazima weusi wameelezea wasiwasi wa kushambuliwa na wazungu, wao au mmoja wa jamaa zao, kwa sababu ya rangi ya ngozi yao nyeusi.

Asilimia 78 ya Wamarekani weusi walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wamesema kuwa hawawaamini hata kidogo watu weupe.

Kulingana na uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na gazeti la Washington Post kwa kushirikiana na taasisi ya Ipsos, raia weusi wa Marekani wanasema kuwa utoaji wa huduma za umma kwa watu wa jamii yao nchini Marekani umekuwa duni na unapungua tangu 2006.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *