2022; mwaka uliokuwa na joto kali sana katika historia ya Uingereza

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Uingereza imeutangaza mwaka 2022 kuwa mwaka uliokuwa na joto kali sana katika historia ya Uingereza.

Kwa mara ya kwanza hali ya joto nchini Uingereza ilifika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa nchini humo ambapo kiwango cha joto kilivuka nyuzi 40.

Takwimu zinaonyesha kuwa, kuanzia mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu, watu 3,271 waliripotiwa kuaga dunia kutokana na joto kali huko Uingereza; idadi ambayo imepindukia wastani wa vifo vilivyoripotiwa miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, aghalabu ya watu waliopoteza maisha ambao walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 65 waliaga dunia mwaka huu  katika siku ambazo kulikuwa na joto kali sana huko Uingereza. Hali hiyo ya joto aidha ilisababisha kuungua makumi ya nyumba katika mji mkuu na katika miji mingine ya Uingereza.

Sadiq Khan Meya wa jiji la London mwezi Julai mwaka huu aliitaja hali hiyo ya mambo kuwa mbaya na akalinganisha hali ngumu inayowakumba wafanyakazi wa huduma za zima moto na Vita vya Dunia.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *