Wizara ya Ulinzi ya Uingereza yadukuliwa

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba wadukuzi walishambulia seva za Wizara ya Ulinzi ya Uingereza na kupata habari zenizohusiana na maafisa na wanajeshi.

Shirika la habari la B B C limeripoti kuwa mfumo huo uliodukuliwa ulikuwa na majina na taarifa za benki za wafanyakazi wa sasa na baadhi ya wafanyakazi wa zamani wa Jeshi la Uingereza.

Kulingana na ripoti hii, inawezekana kwamba anwani za baadhi ya askari wa jeshi pia zilidukuliwa.

Bado haijabainika ni nani anayehusika na udukuzi huu, lakini inasemekana kwamba habari iliyodukuliwa inahusiana na wanachama wa sasa na wa zamani wa Jeshi la Wanamaji la Uingereza, Jeshi na Jeshi la Anga.

Mfumo huo ambao ulidukuliwa unasimamiwa na mkandarasi nje ya Wizara ya Ulinzi ya Uingereza na taarifa za uendeshaji wa wizara hii hazikudukuliwa.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza iliondoa mfumo uliotajwa mara moja na uchunguzi katika uwanja huu unaendelea.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Grant Shapps anatakiwa kuwafahamisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu tukio hili leo na kutoa taarifa zaidi.

Tobias Ellwood, mbunge wa Conservative na askari wa zamani, aliiambia Sky News: “China labda inaangalia watu walio katika mazingira magumu kifedha ambao wanaweza kufanya kitu kwa pesa.”

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *