Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Imewtolewa katika: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 10 May, 2024
Hotuba ya 1: Tafsiri isiyo sahihi ya Tawassul imeunda dini nyingine dhidi ya Quran
Hotuba ya 2: Vijana wa Pakistan wanapaswa kuifanya Pakistani kuwa uwanja wa kuinuka kwa ajili ya Wapalestina
Msisitizo juu ya Taqwa ndio ulio zaidi ukilinganisha na maamrisho mengine ya ibada. Katika Surah Maida, aya ya 35, uwanja mmoja zaidi wa Taqwa umewekwa na Mwenyezi Mungu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {35}.
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia za kujikurubisha Kwake, na piganeni Jihadi katika Njia Yake ili mpate kufaulu.
Kuna amri tatu katika aya hii, hotuba moja na tija moja. Hotuba ni kwa waumini ambayo ni hatua ya msingi ili kuweza kuelewa aina ya mwongozo. Hotuba ya Quran ni kuelekea jamii ya waumini. Enyi mlioamini maana yake jamii inayohutubiwa ni ile ambayo imeanzishwa kwa misingi ya imani. Jamii zinaweza kuwa na misingi kadhaa kama vile uchumi, ustawi, elimu, kazi, hali ya hewa, makabila, rangi n.k. lakini kwa ujumla jamii za leo zimeegemea kwenye maslahi binafsi ya binadamu na jumuiya. Hazizingatiwi kama jamii za waumini. Leo watu katika Lahore wanaishi pamoja kwa msingi gani? Ni kwa mambo mengine yasiyokuwa imani na itikadi. Hakuna anayeweza kusema kwamba nimekuja Lahore kwa itikadi na imani yangu. Kuna mtu amekuja kwa ajili ya elimu, jamaa, jumuiya n.k. Jamii ya waamini imejikita katika maadili ya kawaida yanayohusiana na imani na maisha yao yanasimikwa katika imani. Dhana ya imani (Iman) iliyopo katika akili zetu sio maana ya Qur’an bali ni ya kielimu ambayo ina maana ya kuamini tu kwa moyo na kushuhudia kwa ndimi kwamba kuna muumba. Uhusiano nilio nao na Mwenyezi Mungu si sehemu ya imani yetu. Ni dhana tu akilini lakini Quran haiwazingatii wale wanaodai kwa ndimi kuwa ni waumini. Sisi ni waumini kwa kuzaliwa, kibaolojia au kwa utamaduni. Imani katika mtazamo wa Qur’an ina maana kwamba katika maisha yako binafsi, maisha ya kijamii mambo ambayo unategemea au kuchukua msaada kwa ajili ya kusimamia mambo yako ni imani. Imani juu ya Quran maana yake ni kutegemea Quran lakini badala yake tunachukua tu utulivu wa kiroho kutoka katika Quran. Hatuchukui amri, sheria kutoka kwenye Quran ili zifanyia kazi katika maisha yetu. Tunapata amani na utulivu kwa kusoma tu Quran. Imani maana yake ni ule ukweli ambao Mwenyezi Mungu ameuweka kwa ajili yako, akafungamanisha mambo hayo na wewe na akakuamuru utegemee ukweli huo ili uweze kutekeleza mambo ya maisha yako. Jamii kama hiyo ndio inayo hutubiwa.
Kisha kuna amri tatu; ya kwanza ni kupata Taqwa, kutafuta ukaribu na kisha kufanya Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kutokana na hili waumini watapata Falaah (mafanikio). Waumini wasipofanya mambo haya matatu, hawatafanikiwa kamwe. Uwanja wa Taqwa hapa ni ule uwanja wa mafanikio (Falaah) ambapo yanaweza kupatikana kwa vitendo vingine viwili.
Tumeifafanua Aya katika muktadha wa kutafuta njia kwa namna ambayo tumepata njia ambazo zimetuweka mbali na Mwenyezi Mungu. Maana ya “Waseela” (inamaanisha) haijaelezwa kwa usahihi. Hakuna hata mmoja katika fasihi ya Kiarabu aliyeandika kwamba Taqwa maana yake ni woga au kujiepusha na wote wameandika kwa kauli moja kuwa maana yake ni ulinzi, lakini wanapoingia kwenye Qur’an, wanaifasiri Taqwa kama hofu au kujiepusha na jambo ambalo linajiweka mbali na Qur’an.
Waseela katika fasihi ya Kiarabu (waw, sin, Lam), kuna Wasl zaidi ya moja ambayo ina Swad badala ya sin. Wakati Wasl inapokuwa na swad basi inamaanisha kuunganisha kitu kimoja na kitu kingine. Faṣl ina maana ya kukata na Wasl ina maana ya kuunganisha. Wakati Wasl inapokuwa na Sin, inamaanisha ukaribu, ukaribu. Wataalamu wengine wanasema kwamba Wasl ina maana ya ukaribu na Raghbat (tamaa kali). Tunafanya mambo mengi kutokana na shinikizo, kwa kulazimika na si kwa matamanio makubwa. Mambo hayo yanayofanywa bila Raghbat hayana manufaa. Mambo mengi tunayofanya yana shinikizo kama vile watoto kusoma kutokana na shinikizo la wazazi. Ujuzi huingia ndani ya mwanadamu tu wakati anapokuwa na Raghbat. Dawa huathiri hata ikichukuliwa bila kutamani lakini haitumiki kwa ajili ya kuta mwongozo na ulezi. Watu fulani wanapewa malezi bora zaidi lakini haiwaathiri kwa sababu hakuna Raghbat ndani yao. Raghbat (mielekeo yenye nguvu, tamaa) hufanya kazi kama udongo na maji katika kulea (Tarbiyat). Wakati mwalimu anapanda mbegu ya elimu na kukuza (Tarbiyat) basi Raghbat hupanda mbegu nyingine, na mafundisho yote, elimu, Tarbiyat vyote hivi havina athariy ikiwa itakosekana Raghbat. Hata kwa watu wanaofanya mema, kusikiliza mihadhara kwa ajili ya kupata Thawāb (thawabu). Wale wanaosikiliza hata mambo mazuri yanayosemwa pia hayawaathiri kwa sababu hakuna Raghbat ndani yao.
Katika Dua ya Imam e Zamani (atfs), kwa ajili ya wanafunzi wa elimu anasema , wape juhudi na Raghba katika masomo yao. ikiwa hakuna Raghba basi dini yote kwa ujumla itapotea kwao. Uzoefu huu sisi sote tunao Pamoja na mimi tangia kipindi cha kuwa wanafunzi. Nimepata uzoefu wa kufundisha wanafunzi wa aina zote mbili. Wale waliokuwa na Raghba walisikiliza na walipata maendeleo, lakini wake ambao hawakuwa na Raghba hata baada ya kusikiliza mihadhara yangu waliendelea kubaki kama walivyokuwa kabla. Wanafunzi wanaposoma kwa ajili ya kufaulu mitihani hili haliwasaidii.
Ikiwa Raghba inatengeneza ukuruba basi hii inakuwa ni Tawassul. Kama ilivyo katika jamii yetu kuna aina mbili za ndoa. Aina ni ile ambayo familia huandaa na kuweka mipango na kijana na msichana wote hushiriki katika mipango. Na aina ya pili ni ndoa ya kulazimishwa haisihi. Hata kama kijana na binti walioana kwa kukubaliana lakini hakukuwa na Raghba baina yao kwa wote wawili au mmoja wao alikuwa na raghba kwa mtu mwingine ambapo hawakuweza kuoana. Hivyo akaoa sehemu nyingine bila ya Raghba. Kwa hapa kutakuwa na ukuruba lakini hakuna Raghba. Panapokuwa na ukuruba ambao umekuzwa na Raghba hii ndio inakuwa maana ya Tawassul.
Allah anatoa amri ya kutafuta Taqwa . Ibtigha maana yake ni kutafuta bila ya kupumzika bila kuachana kufanyika kwa juhudi za kivitendo hadi kufanikiwa kufikia malengo. Tafsiri ya Aya inayofanyika ni kwa ajili ya kupata njia au nyenzo ambayo itaweza kukuweka karibu na Allah. Kisha ndani ya Tafsiri za Aya hii utakuta kuwa dini kamili imeendelea kuwa na maana tofauti na ya Qur’an. Tawassul haina maana ya kumpata kiongozi wa kiroho au shakhsia ambayo inaweza kutusogeza karibu na Allah. Kwa mujibu wa Aya hii Allah amefunga milango yote ya kuwa karibu naye moja kwa moja kwa sababu ametutaka tutafute njia na nyenzo za kutukurubisha kwake. Milango ya Mwenyezi Mungu ipo wazi kwa kila binadamu hata kwa muhalifu, mtenda madhambi na hata maadui wa Allah. Pindi anapotubia na kurudi kwa Allah basi milango ya rehema , msamaha na kuomba samahani haifungwi kwake. Allah aliwatuma waongozaji na mitume na hii sio eti kwa sababu milango ya Allah imefungwa, lakini badala yake ni kwamba watu ndio hawafahamu milango hiyo. Allah amewatuma walimu ambao hawakuja kukupeleka kwenye milango iliyofungwa , lakini walikuja kwa ajili ya kukulea wewe ili uweze kuwa na uwezo wa kufanya safari mwenyewe ya kupita milango hiyo iliyo wazi. Mitume na wasomi maulama wanalea uwezo wako na kukufanya uwe na uwezo wa kufanya safari kupitia elimu na malezi (Tarbiyat). Na hakuna yeyote ambaye kwake milango ya kumkurubia Allah imefungwa. Hii sio kwa kuwa maulama huwa 3wanasema kuwa Allah amefanya hivi kutokana na huruma, lakini badala yake ni kwamba hili ni moja ya wajibu wake kama mola kwa wale alio waumba, anawaonyesha njia, na kuwapa kila mahitaji yao ikiwa ni sehemu ya uungu wake.
Kuna sera ya neema ( Qaydatu lutf) ambapo Mwenyezi Mungu amefanya kuwa lazima kwake kutoa njia za mwongozo na kuzikuza kwa ajili ya viumbe wake. Viumbe ambavyo Allah ameviumba ameandaa nyenzo zote kwa ajili ya viumbe vyake, uongofu na ukuaji n.k. ukiutazama mwili wako uatona kila kiungo kina chakula chake, kama mifupa ina chakula cha aina mbali mbali, misuli ina chakula tofauti, jicho lina chakula tofauti na kila kiungo kina chakula tofauti. Leo hii Sayansi zimegundua na kuvipa majina maalumu kama vitamini, madini na virutubisho. Kwa namna Allah alivyo tengeneza kitu ndani ya mwili amekitengenezea chakula chake. Hivyo hivyo kwa ajili ya mwongozo wa mwanadamu Allah ametengeneza nyenzo na utoaji kulingana na kitu. Na haimaanishi kutafuta ukuruba kwa Allah tunahitaji nyenzo ya kati. Allah anakijua kila kiumbe vizuri, na Allah ametuma njia ya kuwaongoza kama Musa ili awaongoze, awape ufahamu, awafundishe ili waweze kufanya safari wenyewe. Mitume hawampeleki kila mtu kwa Allah na kumuomba Allah amsamehe.
Tumemuweka Allah mbingu za mbali ambazo hakuna mtu anayezijua. Kuna msongamano wa malaika baina ya Allah na viumbe wake ambao w2anafanya safari ndefu. Huu ni ufahamu mbaya kuhusu Mola. Qur’an inasema Mola wenu yupo karibu sana na nyinyi wenyewe. Leo kwa ajili ya kutaka ukuruba kwa Allah unahitaji nyenzo. Na nyenzo hizi ni watu ambao wamewaweka watu mbali na Allah na wenyewe kuwa mabwana. Watu huwaabudu. Qur’an inasema tafuta ukuruba kwa Allah kwa Raghbat, au kukuza Raghbat ya kutaka ukuruba kumuelekea Allah. Matamanio yetu yamechosha robo nzima ya Raghba ndani yetu. Hatujabakiwa na Raghba kwa ajili ya Allah. Kuza Raghba kwa ajili ya ukuruba na Allah na hii ndio injini kubwa ambayo humshawishi na kumsukuma mtu kusimama kwa ajili ya Allah. Ibada iliyoambatana na nia na Raghba ni yenye faida. Kwa kupitia kuwa na Raghba pata ukuruba kwa Allah. Taqwa , Ibtighaul Waseelah na jihadi ni amri tatu ndani ya Aya ambazo ukizifuata ndio utapata mafanikio ( Falaah).
Hotuba ya 2
Leo hii tunaweza kuona kwa kuk0sa Taqwa kila mtu kapoteza ubinadamu. Kila mtu inabidi kuthibitisha utu wake na moja ya kigezo na sababu ya haya ni dhuluma inayofanywa ndani ya Palestina. Wanatakiwa kuwaadhibu madhalimu, wawachukie na kuwaonyesha hatima yao. Eneo ulimwenguni ni chungu ndani ya Gaza na ulimwenguni kote. Tunaweza kuona aina za watu mbali mbali ulimwenguni wanaopaza sau5ti zao katika maeneo mbali mbali vikiwemo vyuo vikuu vya Amerika na Ulaya. Zilikuwa ni sauti zenye nguvu kiasi kwamba madhalimu walilazimika kuwasikilizana Wapalestina wameeleza kuridhika kwao nao. Viongozi wa Amerika waliathirika. Sauti bado inaendelea licha ya kuwa kuna ukandamizaji wa madhalimu ambao unaendelea kufanywa.
Anguko kubwa ambalo lipo kwenye ulimwengu wa Kiislamu ambalo ni jina tu lakini hakuna marejeo kwa ajili ya hili. Marejeo kwa ajili ya Uislamu ni wale ambao hawana ubinadamu. Nchi za Kiislamu 58 zote zimekubali jinai na uhalifu unaofanywa dhidi ya Wapalestina. Maulama licha ya kusoma dini lakini bado hawana ubinadamu kwa sababu ya hakuna Taqwa. Leo hii Ijumaa watu huhudhuria msikitini kwa wingi hasa Ahlu Sunna waljamaa na misikiti hujaa na kukosa nafasi. Lakini Ijumaa hupita bila ya kupaza sauti ya kulaani dhuluma inayotendwa na madhalimu. Kama anavyosema Imam Ali (‘a) kwamba wao ni miili iliyojikusanya sehemu moja, lakini nyoyo zao hazipo pamoja hazina umoja. Sio umma wa Kiislamu bali ni watu wa chini wanyonge. Ni udhalilishaji kiasi gani katika zama hizi za teknolojia, ambapo vyombo vya Habari vinaweza kushuhudia aina hizi zote za dhuluma na kila mmoja akabaki kimya. Hii ni dini ambayo walifundishwa bila ya Taqwa.
Unaweza kuona fedheha. Wameiangamiza Gaza, Khan Yunis ambapo watu 40000 wameuawa kishahidi na watu hawa walioharibiwa kila kitu chao wamekimbilia Rafah karibu na mipaka ya Misri. Israel imewashambulia wakimbizi ndani ya Rafah. Wameweka sharti kwamba kama Israel haitashambulia Rafah basi na wao watawaachia huru mateka. Hii ni fedheha kubwa kwa Misri, Qatar, Jordan ambao walikubaliana makubaliano haya ya kuwaachia huru mateka ikiwa dhalimu hatashambulia. Sasahivi nchi hizi zinashirikiana na Israel kumzingira Iran. Hamas wamepewa amri ya kuondoka Qatar. Hamas na Wapalestina hawapo tayari kuachia mateka na kukata tamaa. Kuharibu miji, kuua wanawake na Watoto sio kushinda vita bali ni jinai za vita. Hamas wamepigana vita yenye mafanikio na athari zake zinaonekana. Usaliti mwingine uliofanyika ulikuwa chini ya uongozi Saudia ambapo na Pakistan ni sehemu ya usaliti huo. Imam wa Haram Makkah ametoa Hotuba ya kwamba vita inayo endelea Gaza ni fitina na Waislamu wanatakiwa kujiweka mbali nayo. Wanatangaza kongamano la umoja wa Kiislamu ili kutoa akili za watu kwenye suala la Gaza kitendo ambacho kimelaaniwa hapa Pakistan. Jambo la tatu n I kongamano lililopangwa na OIC juu ya anwani phobia ya Kiislamu. Modi anafanya phobia ya Kiislamu kila siku lakini hawazingatii na kuitazama kwa makini. Hawaiti mkutano kiwa ajili ya Gaza. Hizi ni njia za upotoshaji. Amerika inasema ikiwa Israel atashambulia Rafah hatutaipa silaha. Hivyo kwa miezi saba wamekuwa wakitoa silaha kuipa Israel kama ilivyokuwa Uturuki ikiunga mkono Israel kwa miezi saba. Shinikizo juu ya Israel linatokea Iran, Hizbullah, Yemen na baadhi ya sehemu nyingine chache zilizofichwa mfukoni. Shinikizo hili sio kubwa kiasi kwamba serikali yao kupata shinikizo.; serikali ya Pakistan inajaribu kuifurahisha Amerika kila siku, wanatoa silaha kwenda Israel kupitia wafanye biashara wa silaha mbele ya macho ya serikali. Jenerali Zai ul Haqq mkono wake umetapakaa wekundu wa damu za Wapalestina pindi alipokuwa mjumbe huko Jordan. Hawa madhalimu wana mtandao ndani ya Pakistan, wana vituo vya kielimu na maslahi mengine. Taifa la Pakistan, vijana wa Pakistan wanatakiwa kuvunja mtandao huu kwa namna yeyote iwezekanayo na kuibadili Pakistan kuwa ni uwanja wa kunyanyuka na kusimama kwa ajili ya kuwatetea Wapalestina. Waislamu wachamungu wa Pakistan inabidi wapaze sauti zao na kufanya kila wawezalo kwa ajili ya Wapalestina wanaodhulumiwa.