Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa mapema asubuhi ya leo, risasi zilifyatuliwa karibu na Ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Uswidi.
Afisa wa Uhusiano wa Umma wa Idara ya Polisi ya Stockholm aliliambia gazeti la “Expressen” kwamba asubuhi ya leo polisi wa doria walisikia sauti ya milipuko mikubwa, ambayo inaonekana ilitoka kwa bunduki.
Kufuatia tukio hili, vikosi vya usalama vilizingira Ubalozi wa Israel mjini Stockholm baada ya saa 02:00 asubuhi ya leo hadi saa 06:00 asubuhi kwa saa za huko, na uchunguzi unaonyesha kuwa kulitokea ufyatulianaji wa risasi.
Vikosi vya polisi vya Uswidi viko karibu na ubalozi wa Israel na wanatafuta athari za risasi. Afisa huyu hakuzungumzia iwapo ubalozi wa utawala wa Kizayuni ndio ulilengwa kwa kupigwa risasi au la.
Bila kutoa maelezo, alisema kuwa watu kadhaa wamekamatwa katika uchunguzi wa awali kuhusiana na tukio hili.
Huku kukithiri jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ghaza na azma ya Tel Aviv ya kufanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Rafah, wimbi la chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni limeanzishwa kote duniani na kumeanzishwa kampeni nyingi za kusimamisha Gaza. vita.