Kufuatia salamu za rambirambi za viongozi na maafisa wakuu duniani, kufuatia kuuawa shahidi Ayatollah Raisi na viongozi wenzake, Rais wa Kenya alitangaza mshikamano wake na taifa la Iran katika usiku wa kuamkia Jumatatu.
Katika muendelezo wa risala za rambirambi za viongozi na shakhsia wa dunia kufuatia kifo cha rais na waziri wa mambo ya nje wa Iran, Rais wa Kenya William Ruto alitangaza mshikamano wake na taifa hilo Jumatatu usiku saa za Tehran.
Kulingana na tovuti ya “KDRTV”, Ruto alimsifu Ayatollah Seyed Ebrahim Raisi kama rais asiye na woga na aliyejitolea kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Katika ujumbe wake huo amesema: “Kwa kufariki dunia Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir Abdullahian na ujumbe aliofuatana nao, natoa salamu za rambirambi na mshikamano wangu na taifa la Iran katika wakati huu mgumu.”
Helikopta iliyokuwa imembeba Ayatollah Raisi na wenzake ilipata ajali njiani kurejea Tabriz baada ya kufunguliwa kwa bwawa la “Qiz Qalasi” mnamo Mei 30 katika hali mbaya ya hewa.
Mbali na rais, helikopta hii ilikuwa imembeba Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian, imamu wa Ijumaa wa Tabriz Seyyed Mohammad Ali Al-Hashem na Gavana wa Azerbaijan Mashariki Malik Rahmati, pamoja na kundi la walinzi na wafanyakazi wa ndege.
Rais wa Kenya alimtaja Shahid Raisi kuwa rais shupavu aliyetaka kuboresha nafasi ya Iran katika ulingo wa dunia. Ruto alibainisha kuwa serikali yake inasimama pamoja na watu wa Iran.
Cyril Ramaphosa, rais wa Afrika Kusini pia alielezea masikitiko yake na maafisa wakuu wa Iran siku ya Jumatatu.
Ramaphosa alisema: “Ni msiba wa ajabu na usiofikirika kwamba rais wa taifa ambalo Afrika Kusini ina uhusiano mkubwa na nchi mbili na ambaye tulipata heshima ya kumkaribisha kwenye mkutano wa kilele wa BRICS huko Johannesburg mwaka 2023, amefariki dunia.