Kulingana na Rais wa Chuo Kikuu cha Amir Kabir, Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono harakati za wanafunzi wa Marekani wanaounga mkono taifa la Palestina ni jambo lenye kuwapa nguvu na kuwatia moyo wale wapenda uhuru.
Makundi ya muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya kushtukiza maarufu kama kimbunga cha Al-Aqsa kutoka Gaza iliyoko (kusini mwa Palestina) dhidi ya utawala wa Israel mnamo tarehe 7 mwezi wa Oktoba, mwaka 2023.
Tangu kuanza kwa mzozo wa moja kwa moja na kati ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni na vikosi vya Hamas, zaidi ya watu elfu 36 wa Ghaza wameuawa shahidi na zaidi ya watu elfu 81 kujeruhiwa. Habari zilizochapishwa kutoka Gaza zinaashiria jinai za utawala wa Kizayuni katika eneo hili.
Kwa mujibu wa ripoti hii ya vyuo vikuu vya Marekani, tangu tarehe 18 Aprili (30 Aprili 1403), wanafunzi wa Marekani wamekuwa wakishiriki maandamano yenye kulaani vitendo vya utawala wa Kizayuni, na vile vile kudhihirisha umoja wao pamoja na watu wa Gaza kama ishara ya kuiunga mkono Palestina.
Vile vile walitaka marais wa vyuo vyao waunge mkono hadharani usitishaji vita katika mji wa Ghaza, na kwamba wasitishe ushirikiano na uwekezaji katika makampuni ya Kizayuni.
Hali kadhalika wametaka usitishaji wa uzambazaji wa silaha kwa jeshi la utawala huo ghasibu, pamoja na kukata uhusiano wa kielimu kati yao na utawala huo.
Harakati hizi za wanafunzi nchini Amerika zimechochea maandamano katika vyuo vikuu vya nchi nyenginezo kama vile Uingereza na Ulaya n.k. zikiwemo India na Lebanon.
Lakini maandamano haya yamekabiliwa na polisi wa Marekani na matokeo yake wanafunzi wengi wamekamatwa.
Hivyobasi, Ayatullah Khamenei ambaye ni Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika barua aliyowaandikia wanafunzi wanaounga mkono kwa dhamiri zao wananchi wa Palestina katika vyuo vikuu vya Marekani huku akionesha masikitiko na mshikamano wake kwa maandamano hayo dhidi ya Uzayuni. Amewachukulia kama sehemu ya mbele ya upinzani na kuashiria mabadiliko ya hali na hatima ya eneo nyeti la Asia Magharibi, na vilevile alisisitiza kwamba hili litasababisha kugeuka kwa historia ya ulimwengu.
Licha ya kwamba barua hii imezuia hisia nyingi katika mitandao ya habari ulimwenguni, vyombo vya habari vya Kiarabu na vya Kimagharibi vimetilia maanani sana barua hio iliyo na ujumbe mzito na maneno yenye kuongeza hamasa katika suala zima la Mzozo kati ya taifa la Palestina na Utawala dhalimu wa Israeli.