Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(mkuu wa Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Imetolewa : Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 31 May, 2024
Hotuba ya 1: Falah ni nini, na vipi Taqwa, Tawassul na Jihadi humpeleka mtu kwenye Falah.
Hotuba ya 2: Ukatili mbaya sana katika historia ya ubinadamu umefanywa Rafah
Taqwa imeamrishwa katika njia nyingi na maandiko mengi katika nyanja nyingi za maisha. Miongoni mwa amri hizi ni katika Aya ya 35 ya Suratul Maida.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {35}
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia za kujikurubisha Kwake, na piganeni Jihadi katika Njia Yake ili mpate kufaulu.
Katika Aya hii waumini wamepewa amri tatu; Moja ni kutafuta na kupata Taqwa, pili ni kutafuta Raghbat kwa ukaribu wa Mwenyezi Mungu na tatu ni Jihadi (Jihad) katika njia ya Mwenyezi Mungu na kisha matokeo ya haya matatu yanatajwa kuwa ni mafanikio (Falah). Katika aya mbalimbali Falah ametajwa kuwa ni matokeo ya maisha ya mwanadamu. Falah haimaanishi mafanikio badala yake mafanikio ni sifa muhimu ya Falah.
Falah kwa Kiarabu ina maana ya kulima hivyo pia kwa sababu Falah halisi ina maana ya kuipasua ardhi. Mkulima hupasua ardhi ili kuweka mbegu ndani yake. Hii inajulikana kama Falahat ambayo ina maana ya kupasua na kurarua kwa madhumuni ya kupanda na kuvuna. Hii ni ya jumla na inatumika kwa mambo ya kimaada na kiroho. Hii ina maana hutokea juu ya ardhi na pia katika nafsi ya mtu. Mbegu inaweza kuwekwa ndani ya ardhi na pia katika akili, moyo, nafsi na utu. Uwanja au shamba la tatu ambalo mbegu huwekwa ambalo ndilo shamba kubwa lililochaguliwa kwa ajili ya mwongozo na kupuuzwa na sisi ni jamii. Sisi tuko makini kuelekea ardhi na wakati fulani hata kuelekea roho zetu lakini uwanja muhimu ambao Mwenyezi Mungu ameuchagua kwa ajili ya kupanda mbegu muhimu zaidi ni jamii. Katika uelewa na mafundisho ya dini jamii inapuuzwa kabisa ambapo katika mafundisho yasiyo ya kidini jamii inapewa umuhimu mkubwa. Dini imejikita kwenye ubinafsi tu ambayo maana yake tunataka kupanda mbegu ndani yetu binafsi na sio jamii. Aya nyingi zinatuonyesha kwamba watu binafsi wanazingatiwa kama miti ya bustani na wanapaswa kulelewa ndani ya bustani ya jamii na sio kwa kujitenga. Mwelekeo mzima wa dini ni kuelekea hili pekee na si kwamba dini inataka kuotesha mbegu kwenye chungu ambacho kinaweza kutoa urembo fulani. Hakuna mimea au matunda huja kwenye mimea kwenye sufuria. Wasomi wetu wa maadili huchukua mimea kutoka kwenye jamii ili kuipanda kwenye sufuria nyumbani. Masufi na wasomi wa maadili wana mzio kutoka kwa jamii. Ukikabidhi jamii kwao, watachukua mimea michache kutoka kwenye jamii na kuipeleka nyumbani.
Nabii Musa, Nabii Ibrahim, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walitumwa kwa ajili ya wokovu wa Umma. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angezingatia tu kizazi chake na kuwalea kwa kufunga milango ya nyumba yake. Lakini Mwenyezi Mungu hakuwatuma kwa ajili ya hayo. Mtukufu Mtume (saww) anasema kwamba dunia hii ni shamba la akhera na hadithi hii ipo katika vitabu vyote vya Sunni na Shia. Tunapotafuta Hadithi, tunapaswa kutafuta Hadithi nje ya vitabu vya madhehebu yetu pia. Madhehebu fulani yanaguswa sana linapokuja suala la kukubali Hadithi kutoka kwa Ahlulbayt (a) ambao huu ni ugonjwa. Hawachukui hata Hadithi kutoka kwa Makhalifa wanne na hutapata Hadithi nyingi kutoka kwa hawa wanne katika vitabu vyao. Kwa nini? Walikuwa wakiutawala Ummah na kila siku walikuwa wakitoa rejea kuhusu maneno ya Mtukufu Mtume (saww). Huu pia ulikuwa ni mpango wa Banu Umayyah ambao wao walipanga kwamba wachukue Hadith kutoka kwa nani na wasichukue hadithi kutoka kwa nani, kama tu vyombo vya habari nini cha kuchukua na nini cha kuonyesha. Wakati huo vyombo vya habari vilikuwa chini ya udhibiti wa Banu Umayyah na walikuwa wakividhibiti. Hadithi hii imo katika vitabu vyote kwamba dunia hii ni shamba la akhera.
Hadithi hii inawasilisha uhalisia, utambulisho wa dini na kuwasilisha uhusiano kati ya dunia na akhera; huo ni uhai kabla ya kifo na baada ya kifo. Maisha ambayo tunaishi sasa kabla ya kifo tunapaswa kufahamu kuwa tunaishi katika uwanja wa shamba na sehemu ya mazao yanayolimwa shambani. Je, wewe kama mkulima unapaswa kupanda nini? Inakupasa kupanda mbegu ya akhera ambayo itaota hapa duniani tu ambayo utaipeleka Akhera.
Katika Surah Shura (42) Aya ya 20
مَنْ كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَنْ كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ نَصِيبٍ {20}
Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.
Harth maana yake ni shamba. Mwenyezi Mungu anasema dunia hii ni shamba la dunia au akhera. Mwenye kutaka matokeo hapa duniani tunampa hayo lakini hana faida huko akhera. Imani zetu juu ya dunia na akhera ni kwamba kila tunalolifanya Malaika wanaliandika na hakuna ujira wowote ambao ungelipwa duniani lakini utakapokufa basi utapata malipo yote huko akhera. Hii ndiyo dhana yetu ya dunia na akhera, maisha na dini. Sote tumesikia haya kutoka kwa wazazi, shule, wanachuoni lakini tunaposoma Quran tunakuta kuna kitu kingine kimeandikwa ndani yake.
Quran inasema wewe ndiye unayeunda utu wako, ulimwengu na chochote unachofanya hapa ndio akhera yako pia. Matendo yote, miitikio, fikra ni ujenzi wa akhera na sio kwamba akhera hujengwa mapema na Mahuri wamekaa wakiwa ni wenye kukungojea peponi kwa Maulana ( Allah). Kila kitu kinachoamrishwa na Mwenyezi Mungu ili mkifanye na mambo mnayoyafanya peke yenu bila ya kuamrishwa mawili haya yote ni Akhera. Qur’an inataja hili kama Falah. Muflehoon ni kwamba mkulima ambaye amefanya kazi ngumu kuianzisha dunia kwa kupanda mbegu, kuzipanda, kuzilinda na kuvuna. Mufleh si mkulima pekee bali ni yule ambaye amefanya yote haya ili kuvuna mazao na kuyaleta nyumbani. Hii ni tafsiri nzuri ambayo imefanywa na Quran. Na dhidi au mkabala ya Muflehoon ni wenye khasara. Wale ambao hawajalima chochote au wamelima mimea yenye sumu ya mwitu.
Katika aya hii ya 35, Quran inasema jipatieni Taqwa, tafuteni Raghbat kwa ukaribu na fanyeni Jihad yaani toeni uwezo wenu wote katika njia ya Mwenyezi Mungu. Tunapo fundisha mambo haya yote, kama wanafunzi na waumini wengine wanaoendelea kutusikiliza lakini bado hakuna mabadiliko yanayokuja au yanayotokea kwa sababu maana za zamani, dhana zilizopo katika akili zetu bado hazijaondolewa. Tumekuwa tukiwasilisha kuhusu Taqwa tangu miaka mingi lakini bado maana ya Taqwa inayokuwepo kivitendo katika maisha yetu ni woga na kujizuia. Je, tumefanya nini kuhusu Taqwa kama ulinzi. Je, tumejilinda kiasi gani wenyewe?
Falah imebadilisha muundo mzima wa maisha yako ambayo ina maana kwamba unapaswa kuchagua shamba, kulitayarisha, kupanda mbegu, kulima, kukua na kisha kuvuna. Uwanja huu ni uwepo wako mwenyewe, kuwepo lakini si ndani ya sufuria bali uwe katika jamii. Sitawisha mpango wako katika jamii na pia fanya kilimo cha jamii. Panda ndani ya jamii na kisha fanya ukulima wa jamii. Panda mbegu za mwongozo moja baada ya nyingine ndani yako na jamii pia. Unapo mwagilia shamba, hufikia mimea pekee. Jamii inapokua na akili basi mmea huipata. Na ukimwagilia tu mmea maalum tu na kuacha mimea mingine basi shamba litabaki kavu. Bustani, mashamba humwagiliwa maji na kila mmea hunyonya sehemu yake. Katika msimu wa maembe mashamba yote huwa yamejaa maembe.
Unapopanda, kulima kitu ndipo utavuna tu. Ukitaka dini na Pepo ya Mwenyezi Mungu basi hiyo itapatikana kwa kilimo, na kufikia uvunaji katika dunia hii. Dunia hii itakuwa ndio akhera yako. Qur’an inasema mtu ambaye ni kipofu hapa duniani atabaki kuwa kipofu hata akhera pia. Mtu ambaye ni mzembe, asiyekuwa na mafanikio, aliyenyimwa katika ulimwengu huu atakuwa hivyo akhera pia. Laana inayotajwa na Qur’an kwa ajili ya watu fulani inamaanisha kunyimwa ambako kuko kinyume na rehema (Rahmat). Si waliolaaniwa ambao wameapishwa badala yake wamenyimwa vitu ambavyo Mwenyezi Mungu amewawekea. Tumenyimwa dini, mapendeleo, imani, vitendo, jamii, mifumo ya kiungu, Uimamu, Quran na hao ndio waliolaaniwa.
Muflehoon wale wanaopata Taqwa maana yake ni kuishi maisha ya ulinzi na kulinda mashamba yao ya kuvuna. Wale wanaotafuta ukaribu wa Mwenyezi Mungu kwa Raghbat na sio ukaribu wa Mahurul ain. Hata ukipata Mahuri, matunda, asali peponi lakini ukawa hupati ukaribu na Mwenyezi Mungu basi itakuwaje? Basi hujafanikiwa. Imamu Husein (a) anasema aliyekukuta amepoteza nini na aliye kupoteza amepata nini? Ukamilifu maana yake ni kupata ukaribu na Mwenyezi Mungu. Aya ya Raja: Sisi tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na tunakwenda kwa Mwenyezi Mungu. Hujatoka Jannah, umetoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo inakupasa kurejea kwa Mwenyezi Mungu. Kumfikia Mwenyezi Mungu ni Akhera, Falah, kipaumbele kisha tafuteni ukaribu na Mwenyezi Mungu. Raghbat yako yote inaelekea Pepsi na Sprite, ilibidi umfikie Mwenyezi Mungu lakini umefikia fadhila za Mwenyezi Mungu. Pepo iliyo bora zaidi ni Liqaullah, ambayo ni pepo ya Watakatifu wa Mwenyezi Mungu. Ikiwa hamumfikii Mwenyezi Mungu basi wewe utakuwa ni miongoni mwa waliokhasirika.
Hotuba ya2
Kuna unyama unaoonekana kila mahali ikiwa maisha hayana Taqwa. Leo hii kila mtu anaweza kushuhudia kwamba wanadamu wanaishi maisha yao katika msitu wa wanyama wa mwitu wakali. Tunajifanya binadamu lakini hatuwezi kuona ubinadamu popote katika msitu huu. Kila nchi iko hivi tu lakini unyama unaodhihirika wazi zaidi ni kuona katika Palestina na Gaza ambapo kila siku hatua mpya ya ukatili na dhuluma imefanyika. Katika wiki hii ukatili wa kinyama uliokithiri zaidi umefanywa. Rafah mji wa mwisho wa Palestina ambapo Israel ilivamia baada ya kutangazwa na hata baada ya mazungumzo ya ulimwengu wa Kiislamu na hata mahakama ya kimataifa ya haki ilipiga marufuku mashambulizi dhidi ya Rafah na kusimamisha mashambulizi yote lakini bado shambulio hilo lilifanyika Rafah. Unyama huo ulikuwa kwa kiwango kikubwa ambacho Netanyahu pia aliona aibu na kusema kuwa shambulio hili lilifanywa kimakosa.
Rafah ni kambi ya wakimbizi kwenye mpaka wa Misri na Palestina. Ni sehemu ndogo ambayo ni mwenyeji wa waliojeruhiwa, mayatima, wanawake na watu walioachwa kutoka Palestina wamekimbilia katika kambi hizi. Haya yalikuwa mahema ya muda yaliyo tengenezwa kwa kitambaa na yalichomwa moto na watoto, wanawake waliteketezwa wakiwa hai. Waigizaji wa filamu, waigizaji wa Pakistan, India na Amerika wanalaani mashambulizi haya. Ilikuwa ni kitendo cha kinyama kiasi kwamba kategoria hii ya waigizaji wanaoishi katika ulimwengu tofauti ambapo watu wanaoheshimiwa hata hawaendi kuwa karibu nao. Lakini bado walihisi uchungu wa Rafah na mkabala wao tazama ulimwengu wa kidini, wasomi wa Pakistani, ulimwengu wa Kiarabu. Erdogan mhaini alilalamika kwa kushindwa kwa ulimwengu wa Kiislamu kusitisha vita hii. Wewe mwenyewe umekuwa ukitoa silaha kwa miezi saba kwa Israeli hivyo wewe hauhusiki na ulimwengu wa Kiislamu. Shambulio la wiki iliyopita lilikuwa shambulio baya zaidi katika historia na lilikuwa la kikatili zaidi katika kambi hizi. Miili ya watoto wadogo iliyochomwa na kuwa majivu ilitolewa. Ilitolewa katika habari kwamba miili mingi ya watoto ilitolewa ikiwa imekatwa vichwa. Waziri Mkuu wetu ameshukuru kwamba Uhispania imeikubali Palestina. Ikiwa Uhispania imefanya jambo hili zuri kwa nini haujafanya hivi. Ikiwa umefikia suluhisho hili la serikali mbili kwamba angalau zimeikubali Palestina. Hakuna mataifa ya Kiarabu yaliyoikubali Palestina isipokuwa ni mataifa matatu tu yasiyokuwa ya Kiislamu ambayo yamekubali na mengine yote yamebaki yanasifu. Vyombo vya habari vya Marekani vimeeleza kuwa mabomu, silaha zilizotumiwa kushambulia Rafah zilitengenezwa katika kiwanda cha Colorado nchini Marekani. Amerika inachangia kufanyika mashambulizi haya, wamelinda na kutetea shambulio hili na duniani kote shule za Marekani zinaendeshwa, benki za Marekani na biashara zinaendelea.
Mwenyezi Mungu atasikiliza maombi ya hawa waliodhulumiwa. Watu, wasomi, watu wa kidini wa Pakistan wanaweza kuchukua jukumu muhimu. Ulimwengu mzima watu wanaweza kuchukua hatua madhubuti lakini hawafanyi hivyo. Leo Ijumaa hata wale wanaohudhuria sala ya Ijumaa wakiamua wanaweza kusimamisha vita leo. Hii ni hali ngumu sana kwetu kuishi katika ulimwengu wa aina hii. Ni nani walio kimya na ni nani wanaozungumza? Mwanamke mmoja mwenye kujiuza alikemewa na Maulana kuwa unauza mwili wako. Akajibu kuwa nauza mwili wangu lakini siuzi dini na Quran. Hii imethibitishwa ni habari ya kweli. Waigizaji wa Showbiz wanapaza sauti lakini wengine hawafanyi lolote. Nakumbuka katika miaka ya 1980 kikundi chenye silaha kilivamia Kaaba na kufanya shambulio fulani huko. Watu walianza kusema kwamba hili limefanywa na Amerika. Islamabad ulikuwa mji mdogo sana wakati huo, lakini watu bila hata kuchunguza walishambulia Ubalozi wa Marekani na kuuchoma moto. Baadaye ilibainika kuwa haikuwa Amerika iliyofanya hivyo lakini bado watu waliitikia hivi. Lakini leo hii tunaweza kuona kila kitu kimefanywa na Marekani lakini kila mtu yuko kimya, na kwenda Hijja ili kumdanganya Mwenyezi Mungu. Sasa wataleta kondoo, ng’ombe wa bei ghali na kujisikia furaha kwamba tunaifanyia kazi Sunnah ya Ibrahim. Ng’ombe huyu anaweza kukuza akili na hisia lakini huna akili ya kukomesha ukandamizaji huu huko Gaza. Wanakufa, wanaungua na viungo vyao vya mwili vimeungua vimetawanyika. Imamu Khomeini (r.a) alisema kama Waislamu wakimwaga kila mmoja ndoo moja ya maji juu ya Israeli waisrael watazama. Nia hii haipo kwa Waislamu ambao ni msiba mkubwa.
Israeli, Amerika walikuwa wanyama na wanatenda unyama na ukatili. Lakini hawa wasomi wa Kiislamu, wanachodai ni nini na wanafanya kazi gani? Hapa ni hatua ya waumini kufa kwa huzuni na tunapaswa kuyaonea haya maisha ya aina hii. Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa hatuna Taufiq ya kuzuia hili, basi tujaalie kifo na tusiwaone maiti hawa. Wajibu sio kufa bali kusimamisha dhuluma na uonevu huu ambao tumeusahau. Kuna sauti zinazopazwa katika vyuo vikuu vya Magharibi na miili hii iliyoungua itaamsha watu. Wakati watu wa tasnia ya filamu wamekuwa na hisia na akili basi wengine pia watahisi lakini wale ambao walikuwa kwenye Hijja lakini hawaendi Karbala hawataamka kamwe. Tunapaswa kuvunja ukimya huu na chochote tunachoweza kufanya tufanye. Tunapaswa kuonyesha chuki zetu angalau kwenye mitandao ya kijamii. Mwenyezi Mungu hataipuuza miili hii ya watoto wasio na hatia na Mwenyezi Mungu atalipiza kisasi. Ikiwa tuna tabia hii basi pia tutanaswa chini ya kisasi hicho. Mwenyezi Mungu huwapa muda madhalimu na siku moja huwamaliza kabisa. Siku hiyo iko karibu. Hamas wiki iliyopita ilishambulia Tel Aviv katika eneo kubwa. Licha ya uharibifu huu mwingi wako katika nafasi ya kushambulia. Hili ni jeshi la Mwenyezi Mungu lililo salama na Mwenyezi Mungu atawaangamiza Israel kwa mikono ya watu hawa tu. Mwenyezi Mungu atusamehe, atujaalie toba na atukubalie majukumu yetu