Mkuu wa polisi nchini Kenya, Japheth Koome ajiuzulu

Mkuu wa polisi nchini Kenya, Japheth Koome, amejiuzulu huku kukiwa na ukosoaji kuhusu jinsi polisi walivyojibu maandamano ya hivi majuzi dhidi ya serikali yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Katika taarifa, Rais William Ruto ametangaza kukubali kujiuzulu kwa Koome kama Inspekta Jenerali wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi na kumteua naibu wake, Douglas Kanja, kukaimu mara moja nafasi yake.

Aidha Rais Ruto amemteua Eliud Langat kuwa Kaimu Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya.

Koome alichaguuliwa na Rais Ruto Septemba 2022 kushika wadhifa huo.

Hatu ya kujiuzulu mkuu wa polisi nhini Kenya imejiri siku moja baada ya Rais Ruto kufurusha karibu baraza lake lote la mawaziri, akikubali matakwa ya waandamanaji.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na waangalizi wanaoungwa mkono na serikali, wameshutumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya vijana waandamanaji, ikiwa ni pamoja na kufyatua risasi za moto kwenye umati wa watu. Awali Ruto alisema uchunguzi utafanywa kubaini kosa la polisi kwa vifo hivyo.

Maandamano yaliyoongozwa na vijana dhidi ya upandishaji kodi uliopangwa yalianza mwezi uliopita. Baadhi ya waandamanaji walivamia bunge kwa muda kabla ya Ruto kutupilia mbali ushuru huo mpya.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *