Watu wasiopungua 22 wamefariki dunia baada ya jengo la shule kuporomoka Nigeria

Watu wasiopungua 22 wakiwemo wanafunzi kadhaa wamethibitika kupoteza maisha baada ya jengo la shule ya ghorofa mbili kuporomoka katikati mwa Nigeria. Taarifa hii imebainishwa leo na maafisa husika wa Nigeria ambao wamesema zoezi la kuwatafuta watu wengine zaidi ya 100 waliosalia chini ya vifusi vya jengo hilo linaendelea.

Maafisa wa Nigeria wamesema kuwa jengo la ghorofa mbili katika shule ya Saint Academy katika jamii ya Busa Buji katika jimbo la Plateau nchini Nigeria liliporomoka jana muda mfupi baada ya wanafunzi wengi wao wakiwa na umri wa miaka 15 au chini ya hapo kuingia madarasani.

Awali  wanafunzi 145 walikuwa wameangukiwa na vifusi lakini msemaji wa Polisi Alfred Alabo baadaye alieleza kuwa wanafunzi 132 kati ya hao waliotajwa wameokolewa na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali.

Shirika la habari la Associated Press limemnukuu msemaji wa Polisi ya Nieria akisema kuwa wanafunzi 22 wmaethibitika kupoteza maisha. Ripoti ya awali ya vyombo vya habari vya Nigeria ilisema kuwa watu 12 wamepoteza maisha.

Serikali ya jimbo la Plateau imesema kuwa shule hiyo ya ghorofa mbili imeporomoka kutokana na ujenzi dhaifu na mahali ujenzi ulipofanyika yaani karibu na kingo za mto na kuzitaka shule nyingine zenye mazingira sawa na hayo kuzifunga mara moja.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *