Rais Ruto wa Kenya ateuwa wapinzani katika safu ya baraza lake la mawaziri

Rais William Ruto wa Kenya amewateuwa katika baraza lakek jipya la mawaziri shakhsia wa upinzani huku akiwarejesha nyadhifani mawaziri kadhaa aliokuwa amewafuta kazi.

Rais wa Kenya amechukua hatua hii kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali yaliyopelekea kuuliwa watu zaidi ya 50 huko Kenya.

Rais Ruto amemteuwa kiongozi wa wachache bungeni Opiyo Wandayi katika nafasi ya Waziri wa Nishati na akamteuwa mbunge John Mbadi kuwa Waziri wa Fedha. Shakhsia hawa wawili wanatoka katika chama cha upinzani cha ODM cha Raila Odinga.

Uteuzi huu ni wa pili kufanywa hii leo na Rais wa Kenya  ambao umewajumuisha mawaziri wanne na Mwanasheria Mkuu ambaye alimfuta kazi karibu wiki mbili zilizopita. Wiki jana Rais William Ruto alifanya uteuzi wa awamu ya kwanza ya mawaziri 11.

Hatua ya Rais wa Kenya ya kuwarejesha nyadhifani mawaziri wa zamani imekosolewa pakubwa nchini humo. Hivi majuzi Rais Ruto aliwatuhumu watu wasiojulikana wanaoibua machafuko nchini kuwa wanatishia demokrasia ya Kenya kufuatia maandamano yanayoikumba nchi hiyo.

Rais wa Kenya alisema serikali yake haitasalimisha demokrasia ya Kenya kwa watu wasiofahamika  ambao wanafadhili ghasia na machafuko nchini humo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *