Tume ya uchaguzi nchini Uganda yatangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa 2026

Tume ya Uchaguzi ya Uganda (EC) imetangaza ramani ya uchaguzi iliyorekebishwa ikitangaza tarehe ya uchaguzi wa rais na wabunge wa 2026.

Jaji Simon Byabakama, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  amesema uteuzi wa wagombea urais na ubunge utafanywa kati ya Septemba 17 na Oktoba 3, 2025.

Byabakama alisema kampeni hizo zitaanza wiki ya pili ya Oktoba 2025 ambapo upigaji kura wa urais na ubunge utafanyika Januari 12, 2026.

Jumla ya wagombea 11 wa urais akiwemo Rais aliyeko madarakani Yoweri Museveni waliteuliwa na kuwania uchaguzi mkuu wa 2021, huku Museveni akiibuka mshindi kwa asilimia 58.64 ya kura zote zilizohesabiwa.

Museveni mwenye umri wa miaka 79, alimshinda mpinzani wake mkuu, Robert Kyagulanyi, almaarufu Bobi Wine, mwanamuziki maarufu aliyegeuka mwanasiasa. Kyagulanyi alipata asilimia 34.83 ya kura zote zilizopigwa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *