Sheikh Naim Qassim: Njama na mipango michafu ya Israel dhidi ya Lebanon imegonga ukuta

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, njama na mipango michafu ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon imeshindwa na kugonga mwamba.

Faraan: Samahat Sheikh Naim Qassim ameeleza kuwa, Hizbullah katu haitaruhusu uingiliaji wa kigeni katika masuala ya Lebanon.

Kadhalika Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa, harakati hiyo ina hamu na shauku ya kuwa na uhusiano na mataifa yote zikiwemo nchi za Ghuba ya Uajemi, lakini uhusiano huo ujengeke juu ya misingi ya kuheshimiana pande mbili na siyo kwa misingi ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kusema kuwa, mgogoro wa kimsingi na mkubwa ambao unalenga kila kitu ni uwepo wa utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel ambao daima umekuwa ukiitishia Lebanon na kutaka kuikalia kwa mabavu nchi hiyo ya Kiairabu.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, harakati hiyo haitaruhusu katu mipango ya wavamizi kutekelezwa.

Aidha Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, njama na mipango yote ya utawala dhalimu wa Israel itashindwa na kugonga mwamba kama ambavyo hadi sasa utawala huo ghasibu umeshindwa kufikia malengo yake machafu huko Lebanon.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *