Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria alitoa pole kuuawa shahidi Seyyed Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon.
Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema katika mazungumzo yake na wanahabari: Natoa salamu za rambirambi kwa Imam Zaman (A.S.) na Ayatullah Seyed Ali Khamenei, kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu kifo cha shahidi. Seyed Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon. Msiba huu mkubwa ulitushtua.
Sheikh Zakzaky alitoa rambi rambi za kuuawa shahidi Seyed Hassan Nasrallah kwa makundi yote ya muqawama huko Lebanon, Palestina, Iraq, Syria, Yemen na Iran na kwa watu wote huru wa dunia.
Alimpongeza Seyed Hassan Nasrallah kwa kifo chake cha kishahidi na akabainisha kuwa aliishi maisha safi na yenye furaha na kifo chake cha kishahidi kilipelekea mwisho mwema. Namuomba Mwenyezi Mungu amuunganishe na Sayyid al-Shaheda Imamu Husein (amani iwe juu yake).