Imamu Khamenei: Kilichotokea Syria ni matokeo ya mpango wa pamoja wa Marekani na Israel

Kiiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kiilichotokkea Syria ni njama na mpango wa pamoja wa Marekani na utawala haramu wa Israel.

Ayatullah Sayyid Khamenei amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya matabaka mbalimbali ya wananchi katiika Husseiniya ya Imamu Khomeini na kusisitiza kwamba, haipasi kutilia shaka kwamba yaliyotokea Syria ni natija yampango wa pamoja wa Marekani na Wazayuni nan chi moja jirani ya Kiarabu ambayo imekuwa na mchango wa wazi katika hili.

Kionngozi Muadhamu ameeleza kuwa, “Tuna ushahidi ambao unamfanya mtu kutokuwa na shaka katika hili.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuhusiana na muqawama kwamba, harakkati na muqawama wa wananchi utaenea katika eneo lote la Asia Magharibii kuliko ilivyokuwa hapo kabla.

Ayatullah Khamenei amesema, kadiri muqawama uunavyoshinikizwa ndivyo unavyoimarika zaidi, kadiri maadui wanavyotenda jinai ndivyo muqawama unavyokkuwa na msukumo na azma zaidi na kkadiri kunavyoendeshwa vita dhidi yake ndivyo unavyopanuka na kuenea zaidi.

Kadhalika Ayatullah Khamenei amesema kama niinavyoomnukuu: Mimi nawaambia kwamba, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, muqawama na mapambano yataenea katika eneo lote la Asia Magharibi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia: Katika kadhia ya fitna ya Daesh, Daesh yaani bomu la ukosefu wa usalama, Daesh maana yake ilikuwa ni kuivuruga Iraq, kuiyumbisha Syria, kuyumbisha eneo hili, kisha kuja kwenye nukta kuu na lengo la mwisho, ambalo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kuiyumbisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hili lilikuwa lengo kuu na la mwisho. Hii ndio maana ya Daesh.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *