Umaskini na kuzorota kwa maisha ya Waarabu katika jamii ya Kizayuni

Jamii ya Israeli inakabiliwa na changamoto nyingi kama vile ubaguzi wa kijamii na kiuchumi uliokithiri na ukosefu wa usawa, kinyume na mtazamo unaodhihiri kutokana na athari ya propaganda za vyombo vya habari. Waarabu ambao kwamba wanaishi katika ardhi zao wenyewe lakini kutokana na kwamba ardhi hizo zipo chini ya utawala wa Israel nao pia vilevile wanakabiliwa na tatizo la umaskini.

Faraan: Shirika la Usalama wa Jamii la Israeli lilitoa ripoti mwezi Desemba mwaka jana ya kwamba asilimia Hamsini na Tatu nukta Tatu (53.3%) ya Waarabu wanaoishi katika maeneo yaliyomilikiwa kimabavu wako chini ya mstari wa umaskini. Kwa mujibu wa takwimu hizi, asilimia Ishirini (20%) ya Wayahudi wanaoishi katika maeneo ya Palestina yanayomilkiwa kimabavu na utawala wa Israeli, pia vilevile wako chini ya mstari wa umaskini.

Mamilionea wa nchi ya Israeli
Kwa mujibu wa gazeti la Haaretz, mnamo Juni tarehe 22 mwaka wa 2010, wakati mgogoro wa kiuchumi duniani uliposababisha ongezeko la idadi ya mamilionea duniani hadi kufikia kiwango cha asilimia kumi na saba (17%) mnamo mwaka 2009, vilevile idadi ya mamilionea wa Israeli iliongezeka kwa kiango cha asilimia arobaini na tatu (43%) ndani ya mwaka huu. Ongezeko hili kubwa liliiweka Israeli nafasi ya tatu baada ya India na Hong Kong kwa idadi ya mamilionea kwa kila kichwa (yaani, kwa kunasibishwa na idadi ya watu), Kulingana na Haaretz, Hong Kong ilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha mamilionea kwa asilimia mia moja na nne (104%), ikilinganishwa na asilimia hamsini nukta tisa (50.9%) ya India.

Hali kadhalika Marekani, Ujerumani, na Japan zimesalia kuwa nchi zenye idadi kubwa ya mamilionea. Katika mwaka wa 2009, kulikuwa na zaidi ya mamilionea milioni 10 duniani kote, na jumla ya mali ya zaidi ya dola trilioni thelathini na tisa $ 39. Wakati huo huo, Israeli ina mamilionea 8,419. Mwaka 2009 pekee, kulikuwa na mamilionea 83 nchini Israel, 10 zaidi ya mwaka 2008. [2] Hata hivyo, ongezeko la idadi ya maskini ndani ya Israeli ni dalili ya uwepo wa ibada ya pesa na unyakuaji wa haki za wanyonge (maskini).

Ubaguzi katika baadhi ya miji ya Palestina
Jasr al-Zarqa [3] ndio mji wa mwisho uliosalia wa Palestina katika pwani ya Israeli. Ni mojawapo ya miji maskini na yenye watu wengi chini ya utawala wa Israeli. Majengo yaliyosongamana yamejengwa kila mahali katika sehemu iliyosalia, na hamna mti au mmea wowote uliomea katika mji huo. Jasr al-Zarqa ni makazi ya Wapalestina 15,000 na imekuwa ikikabiliwa na shida kubwa ya makazi kwa mda wa miaka mingi. Ardhi zake zimenyakuliwa ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya serikali ya Israeli. [4]

Jumuiya ya wafanyakazi wa Kiarabu na Kiyahudi katika maeneo yaliyokaliwa
Wakati mapengo ya kijamii na kiuchumi kati ya tabaka la wafanyikazi wa Israeli kwa ujumla na utawala wa ubepari ulizidi kudhihirika, ubaguzi ndani ya tabaka la wafanyikazi (haswa kati ya wafanyikazi wa Kiyahudi na Waarabu) ulikithiri. Kwa kuzingatia mapato kama moja ya viashirio vya hali ya kijamii na kiuchumi, wastani wa mapato ya kila mwezi miongoni mwa raia wa Kiarabu katika Israeli mnamo mwaka 2008 ilikuwa kwa shekel mpya ya Israeli 5,419 sawa na kiwango cha dola elfu moja mia nne na sitini na tano za Marekani ($ 1,465). Hiyo ni shekeli mpya 2,530 za Israeli saw ana kiwango cha dola mia sita thamanini na tano ($ 685), au takriban kwa kiwango cha asilimia thelathini na mbili chini Zaidi ikilinganishwa na kiwango cha raia wa Kiyahudi.

Vilevile mnamo mwaka wa 2008, wastani wa mapato ya kila mwezi kati ya wanaume na wanawake wafanya kazi Waarabu ilikuwa takriban 42% na 28% chini, mtawalia, ikilinganishwa na yale ya wafanyakazi wakiume na wakike wanaotokana na Wayahudi katika mwaka huo huo. Hivyobasi, ni wazi kabisa kwamba katika suala la ustawi wa kiuchumi, idadi ya Waarabu wa Israeli iko katika nafasi isiyofaa ikilinganishwa na idadi ya Wayahudi. [5]

Mwandishi: Saeed Abolgazi
[1]. http://parstoday.com/fa/middle_east-i57964
[2]. http://militaant.com/?p=703
[3]. Jisr al Zarqa
[4]. https://www.radiozamaneh.com/440327
[5]. http://militaant.com/?p=703

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *