Ethiopia yaonya: Uhusiano wetu na Marekani unaweza kuharibika

Ethiopia imeishutumu Marekani kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu hali ya usalama, wakati huu inapoendelea na mapambano dhidi ya waasi.

Faraan: Msemaji wa serikali ya Addis Ababa, Kebede Desisa ameonya kuwa iwapo Marekani itaendelea na usambazaji wa taarifa hizo, uhusiano kati ya nchi hizo mbili huenda ukaharibika.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Desisa amesema matamshi ya Marekani yanaumiza pande zote na huenda yakauharibu vibaya uhusiano wao.

Kauli hiyo ya Ethiopia imekuja baada ya Marekani Novemba 5 kuwataka raia wake na wafanayakazi wake wanaofanya kazi ubalozini jijini Addis Ababa kuondoka nchini humo kwa hofu ya mapigano yanayoendelea.

Marekani imekuwa ikiichukulia Ethiopia kama mshirika muhimu wa usalama katika eneo la Pembe ya Afrika lakini uhusiano wa mataifa hayo mawili umeingia doa, kufuatia mgogoro wa zaidi ya mwaka mmoja nchini Ethiopia uliochochewa na vita dhidi ya waasi wa eneo la Tigray ambao wametishia kusonga mbele kuingia Addis Ababa.

Vita hivyo nchini Ethiopia vilianza baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutoa amri ya kushambuliwa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray TPLF baada ya kuwatuhumu wapiganaji wa harakati hiyo kuwa waliwashambia askari wa jeshi la serikali kuu…/

Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *