Al-Nunu ameongeza kuwa, Magharibi imebaini kuwa muqawama wa Palestina ukiongozwa na Hamas umepiga hatua katika kupata uungaji mkono kimatiafa, wakati utawala wa Kizayuni unashindwa kupata uhalali wa kisiasa kutokana na hatua zake za hivi karibuni.
Mshauri huyo wa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, amebainisha kuwa harakati hiyo haitabadili misimamo yake na wala haitashughulishwa na uamuzi wa Uingereza na akongeza kwamba Ismail Haniya ametoa maagizo ya kufanyika uhamasishaji wa kiwango cha juu zaidi wa kutafuta uungaji mkono kwa kadhia ya Palestina hususan katika nchi za Kiarabu…/