Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa moja ya daghadagha za harakati hiyo ni suala la kuachiwa huru mateka wa Kipalestina.
Faraan: Akihutubia mkutano wa uungaji mkono wa Waarabu kwa mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni, Hania amesema: “tunawatangazia mateka wetu kwamba kadhia yao hiyo ni suala linalopewa kipaumbele na ni daghadagha ya muqawama wa Palestina.”
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ameongeza kuwa: kadhia ya Palestina haiwahusu raia wa Kipalestina peke yao bali ni suala linalowahusu Waarabu na wapenda amani kote duniani. Amesema “utawala wa Kizayuni si tu ni adui wetu bali ni adui wenu pia na hatari yake inalihusu eneo zima.”
Ismail Hania ameendelea kusema kuwa “sote tunaona fakhari kwa maamuzi ya baadhi ya nchi kuyaweka majina ya harakati ya Hamas na Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi .”
Hania vilevile ameeleza kusikitishwa na safari ya Benny Gantz Waziri wa Vita wa Israel huko Morocco na kutangazwa kusainiwa makubaliano ya kiusalama kati ya Rabat na Tel Aviv. Morocco na utawala ghasibu wa Israel Jumatano iliyopita zilisaini makubaliano ya kiusalama kati yao wakati wa ziara ya Waziri wa Vita wa utawala huo wa Kizayuni nchini humo.