Israel yapata kiwewe kikubwa cha mashambulio tarajiwa ya HAMAS

Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umeingiwa na kiwewe kikubwa cha mashambulio tarajiwa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS baada ya viongozi wa harakati hiyo kusisitiza kuwa, watatoa majibu makali kwa uchokozi na chokochoko za jeshi la utawala huo ghasibu.

Faraan: Duru za utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel zinaripoti kwamba, vyombo vya usalama na asasi za kijasusi za utawala huo vamizi zinachunguza kwa umakini mkubwa vitisho vya viongozi wa harakati ya Hamas dhidi ya utawala huo.

Baadhi ya vyombo vya utawala huo haramu wa Israel vimeripoti kwamba, viongozi wa utawala huo wanapaswa kuvichukia kwa uzito vitisho hivyo vya Hamas kwani havionekani kama ni vitupu na visivyo na maana na kwamba, katu vitisho hivyo siyo vya kupuuzwa.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz linaripoti kwamba, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limefunga baadhi ya kambi zake za kijeshi zilizoko katika njia zinazoishia huko katika Ukanda wa Gaza likihofia mashambulio ya makombora ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Makundi ya muqawama ikiwemo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS yameupatia utawala wa Kizayuni muda wa wiki moja ili kutekeleza kile kilichofikiwa baina ya pande mbili kuhusiana na Ukanda wa Gaza hasa kuondolewa mzingiro na kuacha kukwamisha mambo kuhusu ukarabati wa eneo hilo, kinyume na hivyo, ujiandae kukabiliwa tena na hujuma na mashambulio.

Katika kipindi cha karibuni, Wazayuni wamekuwa wakifanya njama kubwa za kuwalazimisha Wapalestina waondoke kwenye maeneo yao kama wale wa eneo la Sheikh Jarrah huko Quds, lakini Wapalestina wamesimama imara kulinda ardhi zao.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *