Mkuu wa Harakati ya Kiislamu katika ardhi za Palestina zilizoghusubiwa mwaka 1948 aachiwa huru

Duru za habari zimearifu kuwa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu katika ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu tangu mwaka 1948 ameachiwa huru kutoka katika jela ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Faraan: Shirika la habari la Sama limeripoti kuwa, Sheikh Raed Salah ameachiwa huru leo baada ya kufungwa kwa miezi 28 katika jela ya utawala wa Kizayuni ya Megiddo. Mamia ya wakazi wa mji wa Umm al-Fahm wamemlaki kwa vifijo mkuu huyo wa harakati ya Kiislamu katika ardhi za Palestina zilizoghusubiwa mwaka 1948.

Sheikh Salah alitumia nusu ya kifungo chake cha miezi 28 katika seli ya mtu mmoja ya jela ya Israel.

Utawala wa Kizayuni wa Israel mwezi Novemba mwaka 2015 uliitangaza Harakati ya Kiislamu inayoongozwa na Sheikh Raed Salah kuwa kundi la kigaidi linaloendesha harakati zake kinyume cha sheria kutokana na muqawama na mapambano ya harakati hiyo ya Kiislamu huko Quds inayokaliwa kwa mabavu na katika kutetea Msikiti wa al Aqsa.

Wapalestina zaidi ya 4,650 wanashikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni, 180 miongoni mwao wakiwa ni watoto.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *