Yemen: Tunataka kuwa na uhusiano wa kirafiki na nchi zote isipokuwa utawala wa Kizayuni

Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema, “sisi tukiwa ndio serikali na utawala wa Yemen tunataka kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote isipokuwa utawala wa Kizayuni.”

Faraan: Mahdi al Mashat ameeleza kuwa, Sana’a inataka kuanzisha uhusiano wa kirafiki na nchi zingine zote duniani isipokuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwa msingi wa kutoingilia masuala ya ndani ya Yemen na kuheshimu uhuru na mamlaka yake ya kujitawala.

Al Mashat ameongeza kuwa, propaganda chafu zinazofanywa na vibaraka na mahaini katika ofisi za kidiplomasia za Yemen nje ya nchi zimeitia doa sura ya nchi hiyo na kutoa picha na taswira isiyo sahihi kuhusiana na nchi hiyo.

Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesisitiza kuwa, Wayemeni wako bega kwa bega na masuala makuu ya mataifa ya Kiislamu na maslahi yao ya pamoja ikiwemo kadhia ya Palestina.

Al Mashat amesema, Yemen inaamiliana na Umoja wa Mataifa kwa namna chanya na athirifu na inaitakidi kuwa, taasisi hiyo kuu kimataifa inapaswa iheshimu kujitawala kwa nchi zote na kulinda amani na usalama wa kimataifa…/

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *