Shirika la kutetea haki za watoto: 2021, ni mwaka waliouliwa watoto wengi zaidi wa Palestina

Shirika moja la kutetea haki za watoto limesema, tokea 2014 hadi sasa, mwaka huu wa 2021 ndio ulioshuhudia umwagaji mkubwa zaidi wa damu za watoto wa Palestina.

Faraan: Shirika la kutetea haki za watoto liitwalo +972 Magazine limeeleza katika ripoti yake kuwa, badala ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuwapandisha kizimbani wauaji, unazihujumu shughuli za mashirika ya kutetea haki za watoto wa Palestina na kuyachukulia mashirika hayo kuwa ni ya kihalifu; na likaongezea kwa kusema: 2021 haukuwa sawa na mwaka mwingine wowote.

Shirika hilo limefafanua kwamba, hadi tarehe 14 Desemba mwaka huu, watoto 86 Wapalestina wameuliwa shahidi na askari wa utawala wa Kizayuni katika eneo la Ufukwe wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu, mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu pamoja na Ukanda wa Gaza na likaongeza kuwa, jumla ya watoto 67 waliuliwa shahidi katika mashambulio ya kinyama ya Israel ya mwezi Mei mwaka huu dhidi ya ukanda huo, ambayo yalichukua muda wa siku 11.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya +972 Magazine, katika kipindi cha mwaka huu, askari wa utawala wa Kizayuni wamewaua shahidi kwa kuwapiga risasi watoto15 Wapalestina katika Ufukwe wa Magharibi na Quds inayokaliwa kwa mabavu, kwa kuwalenga moja kwa moja kwa bunduki; na wakawaua shahidi watoto wengine watatu pia mashariki ya Ukanda wa Gaza…/

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *