Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala haramu wa Israel kuhusiana na kushadidisha hujuma na mashambulio yake dhidi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Faraan: Taarifa ya HAMAS imeeleza kuwa, Wazayuni watalipa gharama kubwa endapo wataendelea na huujuma na uvamizi wao katika maeneo ya Wapalestina ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Sehemu nyingine ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa wito wa kushadidishwa muqawama na mapambano dhidi ya hatua za utumiaji mabavu za utawala haramu wa Israel.
Kadhalika taarifa hiyo imebainisha kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kutambua kuwa, katu hautakuwa na amani na utulivu katika ardhi za Palestina.
Vilevile Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa, operesheni za kujitoklea kufa shahidi za hivi majuzi katika mji wa Nablos ulioko katika Ukingo wa magharibi wa Mto Jordan zimetoa ujumbe wa wazi kwa adui Mzayuni.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, viongozi wa Hamas wamekuwa wakitoa indhari na kusisitiza kwamba, kwa sasa harakati hiyo ya Kiislamu ina nguvu kubwa za kijeshi ambazo zinaiwezesha kupiga popote katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.
Wapalestina na hasa watoto, wanawake na wazee wameendelea kukumbwa na masaibu na mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa Israel huku Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zikishindwa kuchukua hatua za kivitendo za kuzuia jinai hizo.