Harakati ya Jihad Iislami ya Palestina imetangaza kuwa kutiwa mbaroni maafisa na Mujahidina wa Palestina hakutazuia makundi ya muqawama kuendelea kukabiliana na uvamizi na vitendo vya kiuadui vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Faraan: Harakati ya Jihad ya Islami imesisitiza katika taarifa yake siku ya Jumatatu jana kwamba kuwaandama maafisa na Mujahidina wa Palestina na kuwaweka kizuizini kamwe hakuwezi kudhoofisha azma ya Mujahidina.
Jihad Islami imeongeza kuwa: Roho ya muqawama na mapambano ambayo imeimarika zaidi baada ya operesheni ya Mfereji wa Uhuru na kuvunja uzio wa jela yenye ulinzi mkali ya Gilboa kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, ingali inatokota katika mishipa ya Mujahidina na inaimarisha azma na nia yao katika njia ya Jihadi na mapambano.
Harakati ya Jihad ya Islam sambamba na kupongeza oparesheni za kjitoa mhanga za “Jenin” na “Silat al-Harithiya”, imewataka vijana wanamapinduzi na Mujahidina wa Palestina kuunda makundi katika maeneo yote ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi na vitendo vya kiuadui vya utawala wa Kizayuni.
Vijana wa Kipalestina wamepambana na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliokuwa wamevamia kitongoji cha Silat al-Harithiya huko magharibi mwa Jenin ambapo askari 3 wa Kizayuni wamejeruhiwa vibaya. Vyombo vya habari pia viliripoti jana Jumatatu kwamba wanajeshi watatu wa Kizayuni walijeruhiwa katika mji wa Jenin wakati wa mapigano ya silaha na wanamapambano wa Kipalestina.