Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC alisema:Leo hii, ikiwa kauli mbiu ni kuifikia Quds Tukufu na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutafika, na lengo hili ni lengo lenye uhakika.
Na lengo letu kuu katika hatua hii ni kuifikia serikali ya ulimwengu ya Hazrat Mahdi (as) na kufikia uwepo wenye baraka wa Imamu wa Zama, na njia hii bila shaka itakua ni yenye kuendelea.
Jenerali Ismail Qaani, ambaye ni Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC, alisema katika sherehe ya kumbukumbu ya mashahidi waliokua walinzi wa Haram Tukufu iliyofanyika mjini Tehran:Njia ambayo mashahidi wetu wenye vyeo na utajo wa juu walikuwa wakiiendea na bado wanaendelea, ndiyo njia ya heshima na ya fahari na ndiyo njia ya yenye baraka za mashahidi, waliinua bendera yetu juu sana na sisi kama wafuasi tunajivunia kwamba viongozi wetu wote waliuwawa kishahidi bila ya ubaguzi, na ikiwa tunataka kuendeleza njia hii basi inamaana ya kwamba tuendeleze njia ya maimamu wetu watukufu ambao nao pia vilevile waliouwawa kishahidi.
Aliongeza kua: “ikiwa tunataka kuendeleza njia ya mashahidi,Tunahitaji kuona jinsi walivyotenda na kutoa fidia vile walivyovithamini maishani maishani vilivyokua na thamani yakidunia na na ya kiroho.Inabidi tuweke mifumo hii mbele yetu na tuishi na kutenda kwa mtindo na njia sawa.
Jenerali Qaani aliendelea kusema: Iwapo kauli mbiu ya ndugu zetu katika ulinzi wa eneo takatifu ilikuwa kwamba siku moja waweze kufika Karbala, Leo hii, ikiwa kauli mbiu ni kufikia Quds Tukufu ambayo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutafika, basi hili bado ni lengo lenye uhakika, na lengo letu kuu katika hatua hii ni kufikia serikali ya ulimwengu ya Hadhrat Mahdi (a.s) na kuufikia uwepo uliobarikiwa wa Imamu wa Zama (a.s) njia hii bila shaka itakua ni yenye kuendelea.Akiwahutubia maadui, kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC alisema: “Nyinyi ni wadogo mno kuweza kufahamu kilichopo ndani ya utamaduni tajiri wa Uislamu na Ushia.”Hakika nyinyi hamuelewi maana ya kifo cha kishahidi. Je, mnafikiri njia hii itakoma kwa kutuulia mashahidi wetu? Je mnaelewa ni kosa gani mlilofanya la kumuua Qassim Suleimani? Mlifikiri ya kwamba kwa kumuua Shahid Suleiman msafara huu utasimama ? Kama mngekuwa na ufahamu japo kidogo, mungeelewa jinsi vipi Shahidi Soleimani alikua katika njia ya haki na ukweli kwa ajili ya Iran na Uislamu na Umma wa Kiislamu duniani kote, kwa kasi na nguvu zaidi kuliko Sardar Soleimani.Kamanda huyo aliendelea akisema: Sisi ni Waislamu na wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w); Jumuiya ya Kiislamu na ya wale walio huru duniani watalipiza kisasi kwenu kwa kupitia njia mbalimbali ambazo katu hamtowahizisahau maisha yenu yote.
Mwishowe, kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC alisisitiza: njia tukufu ya muqawama itaendelea na upanga wa muqawama ndio utakaoondoa vizuizi na vikwazo vyote vilivyopo dhidi Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran na Uislamu kwa ujumla.