Rais Raisi: Uhusiano wa Iran na Azerbaijan unatokana na imani za wananchi kwa misingi yao ya pamoja ya kidini

Rais Ebrahim Raisi amesema, uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan unatokana na itikadi na imani za watu wa nchi mbili kwa misingi yao ya pamoja ya kidini.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Azerbaijan Zakir Hasanov na akasisitiza kuwa, uhusiano wa Tehran na Baku si sawa na uhusiano uliozoeleka wa pande mbili baina ya nchi zingine.

Seyyid Ebrahim Raisi ameashiria mazungumzo yake na Rais Ilham Aliyev wa Jamhuri ya Azerbaijan pembeni ya mkutano wa jumuiya ya ECO uliofanyika nchini Turkmanestan na akasema: sera za Iran ni kupanua ushirikiano na majirani hususan Jamhuri ya Azerbaijan katika eneo la Caucasia; na kwa kutilia maanani misisitizo iliyowekwa katika mazungumzo hayo na marais wa nchi mbili, mwenendo wa kustawisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara ikiwemo wa upitishaji bidhaa katika nchi mbili, unaendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa zaidi.

Katika mazungumzo hayo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametanabahisha pia kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni adui wa wanadamu na katu hauwezi kuwa rafiki wa mataifa ya Waislamu; na ukweli huo unathibitishwa na uvamizi na uchokozi unaoendelea kufanywa na wazayuni katika eneo na dhidi ya wananchi wa Palestina.

Kwa upande wake, waziri wa ulinzi wa Jamhuri ya Azerbaijan, Zakir Hasanov amesema, kikao na mazungumzo aliyofanya na waziri mwenzake wa Iran yalikuwa yenye faida kubwa kwa ajili ya mustakabali wa ushirikiano wa nchi mbili…/

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *