Faraan – Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa Majid Takht Ravanchi amesema kuwa, Tehran haitoweza kuendelea kuwaunga mkono wakimbizi wa Afghanistan iwapo vikwazo vya kikatili vya Marekani dhidi ya nchi hiyo vitaendelea.
Jamhuri ya Kiislamu imekuwa ikitoa usaidizi mbalimbali kwa wakimbizi wa Afghanistan —wakimbizi huingia kwa maelfu katika ardhi ya Iran kila uchao — huku kukiwa na vikwazo vya kinyama vya Marekani ambavyo “vimezua matatizo makubwa kwa serikali na watu wetu”, Takht Ravanchi alisema siku ya Jumatano akihutubia katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ilivyokua nchini Afghanistan.
Aliongeza kua; “Kutokana na kuwekewa vikwazo vya Marekani, rasilimali zetu za kifedha zimezuiliwa. Ni wazi kwamba, ikiwa jumuiya ya kimataifa itashindwa kutoa msaada wa kutosha kwa watu wa Afghanistan wanaoishi nchini Iran kwa wakati ufaao, hatutaweza, sisi wenyewe, kuendelea na usaidizi wetu kwa wakimbizi wa Afghanistan,”.
Takht Ravanchi alieleza kua; “kwa mara nyingine, tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na hasa nchi zenye wafadhili kutekeleza majukumu yao na kuongeza rasilimali mpya hususan zile za kifedha kwa majirani wa Afghanistan ili kuwasaidia wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao,”
Marekani iliiwekea vikwazo Iran mnamo mwaka 2018 baada ya kuondoka kwenye makubaliano ya mwaka 2015, hatua hiyo ya kujiondoa kwenye makubaliano ilikua kinyume na sheria lakini pia kinyume na makubaliano baina ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu na nchi nyinginezo.
Washington imekataa kabisa kurudi nyuma bali zaidi kulegeza kamba panapo marufuku hiyo hata kwa bidhaa muhimu na za msingi kama vile chakula na dawa, ingawa Azimio nambari 2615 la Baraza la Usalama, ambalo lilipitishwa kwa kauli moja mwaka jana, linaondoa usaidizi wa kibinadamu na shughuli nyingine kutoka kwenye serikali zilizokatika vikwazo.