jinai za muungano wa Saudia dhidi ya wagonjwa; Watoto 3,000 wa Yemen walio na saratani wanakabiliwa na hatari ya kifo

Jinai za muungano vamizi wa Saudia na Imarati zimewakumba wagonjwa wa Yemen mara hii; Kwa namna fulani, mashambulizi ya muungano huo yamesababisha watoto 3,000 wa Yemeni wenye saratani kua katika hatari ya kupoteza uhai.

Katika kuadhimisha Siku ya Saratani Duniani, Dk Taha Al-Mutawakil, Waziri wa Afya katika Serikali ya Wokovu ya Taifa la Yemen alisisitiza kuwa Yemen inaadhimisha siku hii huku ikiwa imevumilia matatizo mengi ambapo idadi ya wagonjwa imeongezeka maradufu kutokana na mashambulizi ya muungano dhalimu kati ya Saudia na Emarati.

Mtandao wa Habari wa Al-Masira uliripoti, ukimnukuu Waziri wa Afya wa Yemen, kwamba zaidi ya wagonjwa 60,000 wamelazwa katika vituo vya oncology na wanakabiliwa na uhaba wa dawa na vifaa vya uchunguzi; Huku idadi ya watoto wenye leukemia ikiongezeka, alingezea kuwa suala hili ni jambo lenye kutia wasiwasi.

Afisa huyo wa Yemen aliendelea kusema kua : “Zaidi ya watoto 3,000 walio na saratani wamo katika hatari ya kifo hali hii ikichangiwa na uvamizi kutoka kwenye muungano dhalimu baina ya Saudia na Imarati. “Zaidi ya watoto 2,000 wenye magonjwa ya kuambukiza wanakosa au kunyimwa huduma muhimu za afya.”

Saudi Arabia, ikiongoza muungano wa Waarabu unaoungwa mkono na Marekani, imeanzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen na kuweka vikwazo vya nchi kavu, vya anga na vya baharini tarehe 26 Aprili 2015, ikidai kuwa inajaribu kumrejesha rais aliyejiuzulu wa Yemen kwa nguvu.

Uvamizi huo wa kijeshi haujaweza kuhakiki lolote katika malengo ya muungano wa Saudia bali ulisababisha mauaji ya wanadamu na kujeruhi makumi ya maelfu ya Wayemeni, kuwafanya mamilioni ya watu kuwa wakimbizi, nakusababisha uharibifu wa miundombinu ya nchi hiyo na ueneaji wa baa la njaa na magonjwa yenye kuambukiza.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *