Sheikh Maher Hammoud; Imam Khamenei ni kiongozi wa kihistoria

Sheikh Maher Hammoud, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama amesema katika mahojiano kwamba Imam Khamenei ni kiongozi wa kihistoria.

Sheikh Maher Hammoud, katibu mkuu wa Muungano wa Wanazuoni wa Muqawama nchini Lebanon amezungumza na Radio Al-Noor kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran siku ya Alhamisi.

Katika mahojiano na ‘Al-Siyasah Al-Youm’ , Sheikh Maher Hammoud alisema: “Imam Khamenei ni kiongozi wa kihistoria ambaye kila neno na msimamo wake vimehifadhiwa.”Mwenyezi Mungu aliamuru kuendelea kwa njia hii baada ya kufariki kwa Imam Khomeini (r.a).”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa upinzani aliongeza kwa kusema: “Kilichonivutia kutoka kwa Imam Khomeini ni wakati hatua ya mapinduzi iliposhinda na kuchukua hatamu. Yanayosimuliwa kumhusu huleta mazingatio na yenye kutia moyo. Alikuwa kiongozi wa Kiislamu aliyesimama dhidi ya Marekani na Israel.”

Vilevile Katika mahojiano maalum na Shirika la Habari la Fars, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama alisisitiza kuhusu nafasi muhimu ya Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kusema kwamba “Jenerali Qasim Suleimani alipinga wazo la umoja wa Kiislamu katika nyanja kadhaa.”

Sheikh Hammoud alisema kwamba Generali Suleimani ameifanya Quds kuwa katika kipaumbele miongoni mwa harakati zake. Mwanzoni alisema kuwa: “Hakika yeye alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds; Yaani chama chenye dhamana ya kufuatilia suala la Quds. Ambpo “Quds pia ni suala muhimu la Iran ambalo limepewa kipaumbele miongoni mwa masuala mengine yote.”

Vile vile amesisitiza kuwa, kuhusiana na ikhlasi walionayo viongozi wa Iran katika kuunga mkono kadhia ya Palestina, ifahamike kuwa, Tehran ilitoa bajeti kubwa zaidi kwa ajili ya Kikosi cha Quds na ilitumia vijana wake muhimu zaidi na vikosi vyake vya kupigania kwa ajili yake.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *