Magaidi wenye silaha wamevishambulia vijiji viwili katika jimbo la Niger magharibi mwa Nigeria na kuua watu 14 na kuwateka nyara wengine 15.
Gazeti la Tribune la nchini Nigeria limeripoti kuwa, magaidi waliokuwa na silaha jana Jumatatu waliwafyatulia risasi na kuwaua wakazi 14 wa vijiji hivyo viwili katika jimbo la Niger magharibi mwa nchi hiyo sambamba na kuripua mabomu kadhaa. Magaidi hao pia waliwateka nyara watu wengine zaidi ya 15.
Tarehe 9 Januari mwaka huu pia magaidi walilipiza kisasi cha mashambulizi ya anga ya jeshi la Nigeria dhidi ya ngome zao kwa kuvishambulia vijiji 8 katika jimo la Zamfara na kisha kuwaua kwa umati raia 200.
Jeshi la Nigeria katika wiki za karibuni limefanya kila linalowezekana kuyakomboa maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na makundi ya kigaidi baada ya kutokea mauaji hayo ambapo jeshi limefanikiwa kuvikomboa vijiji hivyo na kuwazika wahanga wa mauaji hayo ya kigaidi.
Wenyeji wa vijiji hivyo pia ambao walikimbia nyumba zao wakihofia mashambulizi ya magaidi tayari wamerejea kwenye makazi yao.
Maafisa husika wa eneo hilo awali walitangaza kuwa raia waliouawa ni 58 hata hivyo watu walioshuhudiwa wanasema kuwa watu waliouawa wanapindukia 200.