Mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Yemen Yaendelea Saudia ikiwa mhusika mkuu

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa ndege za kivita za muungano vamizi wa Saudia huko Yemen jana ziliendelea kuyashambulia maeneo mbalimbali ya raia Waisalmu katika mikoa tofauti ya Yemen.

Televisheni ya al Masira imeripoti kuwa, ndege za kivita za muungano vamizi huko Yemen zinazoongozwa na Saudi Arabia jana zilishambulia maeneo ya raia katika mikoa ya Saada kaskazini mwa mji mkuu wa Yemen, Sana’a na Hadhra Maut.

Msemaji wa jeshi la Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree kabla ya mashambulizi ya jana Ijumaa alieleza kuwa, jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen yametungua droni ya Marekani katika mkoa wa Hajjah.

Saudi Arabia huku ikiungwa mkono na Marekani, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi nyingine kadhaa mwezi Machi mwaka 2015 ilianzisha vita huko Yemen na kuiwekea nchi hiyo maskini ya Kiarabu mzingiro wa baharini, angani na nchi kavu.

Mamia ya maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na kujeruhiwa katika vita hivyo vilivyoanzisha na Saudi Arabia na washirika wake na kupelekea Wayemen milioni 4 kuwa wakimbizi.

Si hayo tu, lakini pia wavamizi hao wa Yemen wamebomoa na kuharibu zaidi ya asilimia 85 ya miundomsingi ya Yemen na kuiacha nchi hiyo ikikabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula, dawa za matibabu na matatizo mengine mengi yasiyoelezeka.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *