Waandamanaji wa Pakistan walaani shambulio la kigaidi katika Msikiti Mkuu wa Imamiyah huko Peshawar

Miji mbalimbali nchini Pakistani ilishuhudia maandamano ya kulaani shambulio la kigaidi dhidi ya waumini Mashia huko Peshawar.
Baraza la Umoja wa Waislamu lilifanya maandamano makubwa katika maeneo tofauti ya nchi, hususan katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, wakilalamikia mauaji yakikatili katika Msikiti Mkuu wa Imamiyah huko Peshawar.

Mauaji hayo yalizua hisia na kumbukumbu za msururu wa ugaidi wa kitakfiri.Jambo lililosababisha watu kwenda kutoa madai yao.

Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Waislamu, Bw. Mohammad Kazemi aliiambia Al-Alam ; “Kwa bahati mbaya, serikali ya Pakistan ililaani tu na haikuchukua hatua zozote zile,”. Kwanza tunatoa wito wa uchunguzi na adhabu zisizo na upendeleo kwa wahusika, na fidia kwa familia za wahasiriwa, na kuondolewa kwa madhehebu ambayo yamewalenga wapenzi wa Ahlu Bayt dhidi ya Uislamu nchini Pakistan.

Aliongeza kwa kusema: “Vilevile Tunataka kukabiliana na vyama vya kigeni ambavyo vimeingia kwenye taasisi zetu na kuupa nguvu ugaidi.”

Taj Hussein, mmoja kati ya washiriki wa maandamano, aliiambia Al-Alam: Ikiwa Serikali yetu itashindwa kutulinda basi ni lazima watubainishie ili tuweze kuchukua hatua za kujikinga kwa sababu kinachoendelea ni upuuzi na hatuwezi kuamini mkasa huu mchungu.

Waandamanaji hao wanasisitiza kuwa lengo la mauaji haya; Ni Kusababisha ukosefu wa usalama na kudhoofisha umoja wa wananchi wa Pakistan kwa kuwalenga raia kupitia vitendo vya kigaidi ili kuibua upya vita vya kimadhehebu, na ni lengo ambalo kwamba maadui hawatoweza kulifikia kamwe.

Kinachowaudhi zaidi wananchi ni kwamba, serikali ya Pakistan bado haijachukua hatua zozote za kimsingi kwa ajili ya kukabiliana na mauaji hayo, jambo ambalo linawapa mshtuko mkubwa Wapakistani wote na wapenzi wa Ahlul Bayt (as) kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vilevile Iraq, Yemen na Lebanon. . miongoni mwa mataifa mengineyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *