Maandamano makubwa ya kupinga Israel nchini Uturuki

Wananchi wa Uturuki jana Ijumaa, kwa mara nyingine tena walimiminika mabarabarani katika maandamano ya kulaani ziara tata ya rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini mwao.

Waturuki walioshiriki maandamano ya jana walikuwa wamebeba bendera za harakati za mapambano za Hizbullah ya Lebanon na Ansarullah ya Yemen, na vilevile picha za Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yenye jumbe za kuulaani utawala katili wa Israel, huku wengine wakisikika wakipiga nara za “Mauti kwa Israel” na “Mauti kwa Marekani.”

Wananchi wa Uturuki waliokuwa wamekusanyika katika Medani ya Taksim mjini Istanbul, mbali na kuchoma moto bendera za utawala haramu wa Israel ili kuonyesha ghadhabu zao kwa safari hiyo ya siku mbili ya rais wa utawala dhalimu wa Israel, Isaac Herzog nchini kwao, lakini pia walikosoa vikali njama zozote za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.

Jumatano iliyopita pia, wananchi wa Uturuki walifanya maandamano makubwa ya kupinga na kulaani safari hiyo ya Herzog katika miji ya Ankara, Istanbul, Gaziantep na Burdur.

Rais Isaac Herzog wa Israel amekuwa kiongozi wa ngazi ya juu wa utawala huo haramu kuitembelea Uturuki kwa mwaliko rasmi wa rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan; tangu Waziri Mkuu wa Israel, Ehud Olmert aitembelee nchi hiyo mwaka 2008.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *