Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, amesema kuwa hatamwacha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya iwapo atashinda uchaguzi wa Agosti 9, 2022.
Raila amesema kuwa Rais Kenyatta amekuwa nguzo muhimu katika utulivu wa taifa na uchumi na kwamba yeyote atakayeshinda hastahili kumtelekeza.
Amesema iwapo atashinda uchaguzi ujao ataendeleza uhusiano wake na Rais Uhuru Kenyatta na atamwendea kwa ushauri katika yanja mbalimbali. Amesema Kenyatta pia huenda akahudumu katika nafasi toafuti katika kiwango cha kimataifa.
Raila vilevile alisema kuwa licha ya kwamba hajakuwa katika serikali ya Uhuru, tofauti na yanayoenezwa, serikali yake inajumuisha kila mtu na atafanya kazi na Uhuru hata baada ya kustaafu.
Amekanusha madai kuwa yeye ni mradi wa serikali na akasema kuwa amekuwa na uhusiano mzuri na Uhuru tangu jadi.
Raila ametetea mapatano yake na Rais Kenyatta mnamo Machi 2018, akisema kuwa yaliepusha Kenya machafuko na kusambaratika.
“Baada ya uchaguzi wa 2017, nchi ilikuwa inasambaratika. Alikula kiapo nami nikala kiapo change. Watu walikuwa wanapiga na kuaga dunia lakini baada ya mazungumzo tukakubaliana kwamba Kenya ni kubwa zaidi ya watu wawili,” amesema Raila Odinga.
Wiki iliyopita Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alimwidhinisha rasmi Raila Odinga kama mrithi wake atapostaafu baada ya uchaguzi wa Agosti 9.