Bin Salman augua maradhi ya megalomania

Ushahidi wa kisaikolojia na kisayansi unathibitisha kuwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman, anasumbuliwa na ugonjwa wa kichaa cha kujiona kuwa adhimu na muhimu kupita kiasi (megalomania) na matatizo yanayoambatana na ugonjwa huo.

Wakati wa mahojiano yake marefu ya hivi majuzi na Muhammad bin Salman, mwandishi wa habari Graeme Wood kutoka The Atlantic alifupisha hali ya Bin Salman kwa kusema kuwa anasumbuliwa na megalomania.

Megalomania ni hali ya kuwa na itikadi bandia na njozi, ambapo mtu hutia chumvi katika kujieleza, tofauti na uhalisia wake, akidai kuwa ana uwezo wa kipekee, ni adhimu na mkubwa, au kwamba ana vipaji vya aina yake, au mahusiano muhimu, vitu ambavyo hana na wala havipo.

Maradhi haya humfanya aamini kwamba, anadhulumiwa na watu wengine na kwamba sababu kuu ya kudhulumiwa huko ni kwamba yeye ni mtu mkubwa na muhimu sana.

Kulingana na utafiti wa kimatibabu, megalomania hujitokeza katika aina na sura tofauti, muhimu zaidi ikiwa ni: Daima hushuku nia au matendo ya wengine, kutowaamini wageni, watu unaowafahamu, au wapendwa wako kupita kiasi, na kuamini kwamba una jukumu maalumu au umuhimu ulimwenguni ambao halitambuliwa rasmi, au linalovurugwa na wengine.

The Atlantic haikuwa ya kwanza kumuelezea Bin Salman kama mtu anayesumbuliwa na maradhi ya “megalomania,” bali magazeti kadhaa, ikiwa ni pamoja na Washington Post mnamo 2018, Daily Mail mwaka 2019, na Middle East Monitor mwaka 2020 yalitangulia kufichua suala hilo pale yalipozungumzia mienendo ya kustaajabisha na mwanamfalme huyo wa Saudi Arabia.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *