Suluhu Azindua Filamu Amerika ili Kuimarisha Utalii Nchini Tanzania

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua filamu yake inayolenga kuvutia watalii nchini Tanzania.

Filamu hiyo inayojulikana kama Royal Tour, itazinduliwa Jumatatu, Aprili 18 jijini New York.

Rais Suluhu aliondoka Tanzania Alhamisi jioni kuelekea Amerika kwa ajili ya uzinduzi huo.

Filamu hiyo pia itazinduliwa jimboni Los Angeles, Amerika Aprili 21 na jijini Dar es Salaam nchini Tanzania Aprili 28 na baadaye Kisiwani Zanzibar.

Rais Suluhu alitengeneza filamu hiyo mwaka jana am – bapo alizuru vivutio mbalimbali vya utalii nchini mwake.

Filamu hiyo inamuonyesha Rais Suluhu ambaye ni mhusika mkuu, akiwa katika vazi lake la safari akiwapeleka watalii katika ziara ya kujionea baadhi ya mandhari za Tanzania.

Kupitia filamu hiyo, Rais Suluhu alitembelea maeneo ya vivutio vya Zanzibar, Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani na mbuga za wanyama za Kilimanjaro kama sehemu ya upigaji picha wa Royal Tour.

Filamu hiyo ni sehemu ya juhudi za Rais Samia kuifanya Tanzania ionekane zaidi duniani na kuvutia wawekezaji wengi wa kigeni na watalii kuitembelea Tanzania.

Malengo ya filamu hiyo yamebainishwa kuwa ni kutangaza maeneo na vivutio vya utalii vya Tanzania  kwa hadhira ya kimataifa, kuonyesha na kutangaza vivutio, sanaa na utamaduni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *