Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni viliripoti kikao cha maafisa wa utawala huo na viongozi wa Jordan baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kulenga Msikiti wa Al-Aqsa.
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, kikao cha wakuu wa Jordan na Israel kuhusu Msikiti wa Al-Aqsa kitafanyika kwa kiwango cha juu zaidi.
Tovuti ya Jordan ya Amoun pia iliripoti kwamba mkutano huo utafanyika baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hali na Mandhari ya Msikiti wa Al-Aqsa siku ya Ijumaa yalikuwa kama uwanja wa mapigano baina ya wanamgambo wa Kizayuni na waumini Wakipalestina.
Wapalestina 31 walipigwa risasi za plastiki, na makumi ya wengine waliathirika na gesi ya machozi.