Baada ya kazi ya kuthibitisha barua za kukata rufaa kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema, wabunge hao wa viti maalumu sasa wameitwa ukumbini kusikiliza hukumu yao.
Mchakato wa kuwahoji wabunge hao 19 wa viti maalumu ulianza rasmi katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam ambapo Baraza Kuu la Chadema linaendelea likiwa na ajenda saba ikiwemo kujadili rufaa za wabunge hao.