Jeshi la Israel limekiri kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Al-Jazeera katika mji wa Jenin baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kulingana na uchunguzi uliofanyika kuhusu mauaji ya mwanahabari huyo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, licha ya madai ya maafisa waandamizi wa utawala wa muda wa Kizayuni kwamba Wapalestina ndio wa kulaumiwa kwa kumuua mwandishi wa Al Jazeera, Shirin Abu Aqla, lakini jeshi la utawala huo ghasibu limekiri kuhusika na jinai hiyo.
Gazeti la Haaretz liliripoti jana Alkhamisi asubuhi kwamba, jeshi la Israel baada ya kufanya uchunguzi kuhusu mauaji ya Abu Aqla, lilikiri kuwa alipigwa risasi na wanamgambo wa Kizayuni.
Kwa mujibu wa ripoti hii, uchunguzi unaonyesha kuwa mmoja wa askari wa kitengo cha siri cha Dufdivan aliwekwa katika umbali wa mita 100 hadi 150 kutoka mahali alipouawa shahidi Abu Aqla na makumi ya risasi zilipigwa mbele yake katika operesheni ya kijeshi.
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa mauaji ya watoto lilidai kuwa askari wa kitengo cha Dufdivan walikataa kumfyatulia risasi ripota huyo wa Al-Jazeera, lakini inawezekana kwamba alipigwa risasi kwa bahati mbaya na askari hao wa Kizayuni.
Haaretz iliripoti zaidi: Baadhi ya risasi zilizopigwa na askari wa Kitengo cha Dufdivan zilielekea kaskazini mwa eneo ambalo Shirin Abu Aqla alikuwepo.
Gazeti hilo pia limeandika kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa jeshi la Israel, risasi iliyompiga Shirin ilikuwa ya milimita 5.56, ambayo ilirushwa kutoka kwa silaha ya M16 ya jeshi la Kizayuni.
Wanamgambo wa Kizayuni walimuua mwandishi wa habari wa Kipalestina wa Al-Jazeera, Abu al-Aqla, katika shambulio la kinyama katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan siku ya Jumatano na kumjeruhi Ali al-Samudi, mtayarishaji wa mtandao huo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya watoa wito wa uchunguzi kamili kuhusu mwandishi wa habari wa Palestina wa Al-Jazeera.