Wazayuni wampiga risasi za kichwa kijana wa Kipalestina na kumuua kishahidi

Wizara ya Afya ya Palestina ilitangaza kuwa jeshi la Israel lilimpiga risasi na kumuua kijana mmoja wa Kipalestina huko Nablus.

Kituo cha habari cha Al-Jazeera kiliripoti Jumatano asubuhi kwamba Wapalestina wasiopungua 77 walijeruhiwa wakati wa maandamano na mapigano kati ya Wapalestina na vikosi vya Israel karibu na kaburi la Nabii Yusuf (as) huko Nablus.

Wizara ya Afya ya Palestina pia iliripoti kwamba mmoja wa Wapalestina waliojeruhiwa ambaye alipigwa risasi kichwani na vikosi vya Israel ameuawa shahidi.

Siku chache zilizopita, jeshi la utawala wa muda wa Kizayuni lilimtumia mtoto wa Kipalestina kama ngao ya binadamu dhidi ya gari la kijeshi wakati wa mashambulizi dhidi ya mji wa Jenin.

Jeshi la Kizayuni limetumia kiapo cha woga cha msichana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 16 kama ngao ya binadamu kwa muda wa saa mbili wakati wa kurushiana risasi na wanamapambano wa Kipalestina.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *