Katika muda wa masaa 48 yaliyopita maeneo mbalimbali ya Ufukwe wa Magharibi yamekuwa uwanja wa makabiliano na mapigano makali baina ya Wapalestina na Wazayuni yaliyotokana na upinzani wa Wapalestina dhidi ya ‘maandamano ya bendera’ yaliyofanywa na walowezi wa Kizayuni.
Siku ya Jumapili walowezi wengi wa kizayuni walishiriki katika kile kinachoitwa maandamano ya bendera huku wakilindwa na kusindikizwa na askari za utawala wa Kizayuni wa Israel katika mitaa na barabara za eneo la kale la mji wa Baitul-Muqaddas, hatua ambayo imekabiliwa na jibu kali la Wapalestina na watetezi wa mji huo wa Quds na msikiti wa al Aqsa.
Ripoti za vyombo vya habari vya Palestina zinaeleza kuwa, tangu siku ya Jumapili walowezi wa kizayuni walipofanya maandamano ya bendera, Wapalestina wamepambana na wazayuni maghasibu katika maeneo 191 na kutekeleza operesheni 55 za muqawama zikiwemo za ufyatuaji risasi na urushaji mabomu ya mkono na maguruneti.
Katika mapigano na operesheni hizo, jumla ya askari na walowezi 19 wa kizayuni wamejeruhiwa, ambapo wazayuni wengi walijeruhiwa katika machafuko yaliyojiri katika mji wa Quds.
Katika maeneo 12 ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, wanamapambano wa muqawama wameshambulia vituo vya kijeshi vya na upekuzi pamoja na magari ya askari wa utawala wa Kizayuni; na maguruneti yasiyopungua 35 yalivurumishwa kuelekea vituo vya Israel vikiwemo vya upekuzi katika Ufukwe wa Magharibi na hasa Jenin na Nablus.
Wakati huohuo, Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina limetangaza kuwa Wapalestina wasiopungua 200 katika mashambulio ya siku ya Jumapili yaliyofanywa na wazayuni katika eneo la mashariki la mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Ufukwe wa Magharibi..