Katika mazungumzo ya simu na waziri mwenza kutoka nchini Kenya, Waziri wa Mambo ya Nje alitangaza utayari wa nchi ya Iran kwenye swala la kutuma msaada wa kibinadamu nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na chanjo ya Corona.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa uhusiano na bara la Afrika hususan Kenya na ulazima wa kuwepo ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kenya kuhusiana na baadhi ya vitisho vya pamoja katika uga wa kimataifa kama vile ugaidi na Uharamia.
Akiashiria mwelekeo mzuri wa kukabiliana na janga la corona nchini Iran, waziri Amir Abdullahian alisisitiza utayari wa nchi ya Iran kupeleka misaada ya kibinadamu katika sekta ya dawa, kama vile chanjo nchini Kenya na Afrika kiujuma.
Huku akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje kutoka nchini Kenya kuizuru Tehran, waziri Amir Abdullahian alitaja ushirikiano wa nchi hizo mbili katika majukwaa ya kieneo na kimataifa na akibainisha kua; kuna uwezekano mkubwa wa kupanua mahusiano katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na biashara na sekta binafsi baina ya nchi hizi mbili.
Aidha waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Rachel Omamo amesisitiza umuhimu wa Iran katika mazungumzo hayo ya simu na kutoa wito wa kustawishwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili; akigusia vikao vijavyo vya kamisheni ya pamoja ya nchi hizo mbili, ameeleza matumaini yake kuwa kufanyika kwa tume hii kutapelekea kustawi na kupanuka zaidi uhusiano wa Iran na Kenya.
Katika wito huo, kumejadiliwa suala la uwezeshaji wa masuala ya kibalozi kuhusiana na raia wa nchi hizo mbili, na katika mazungumzo hayo ya simu pande hizo mbili zimejadili kuhusu maendeleo ya hivi karibuni katika mazungumzo ya kuondolewa vikwazo na suala la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kuhusu Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.