Mashambulizi ya hivi karibuni ya kuwalenga watu wengi nchini Marekani yamepelekea watu tisa kuuawa na wengine 27 kujeruhiwa huku ununuzi wa silaha ukiongezeka katika nchi hiyo.
Katika tukio la hivi karibuni, watu sita wameuawa huko Philadelphia jimboni Pennsylvania, na Chattanooga katika jimbo la Tennessee, na wengine 25 kujeruhiwa 25, polisi walisema Jumapili.
Washambuliaji wengi walifyatua risasi kwenye barabara ya Philadelphia ya South Street yenye shughuli nyingi, eneo lenye baa nyingi na migahawa, nyakati za saa sita usiku Jumamosi. Wanaume wawili na mwanamke mmoja waliuawa, maafisa wamesema.
Katika tukio jingine, watu watatu waliuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya shambulio la risasi karibu na baa moja katika mji wa Chattanooga, maafisa wamesema, wakiongeza kuwa watu wawili walifariki kutokana na majeraha ya risasi na mmoja alifariki kufuatia majeraha baada ya kugongwa na gari akikimbia kutoka kwenye eneo la tukio.
Waathirika watatu walijeruhiwa wakati wakijaribu kukimbia na waligongwa na magari, maafisa wa Tennessee wamesema, wakiongeza kuwa wengine kadhaa waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.
Nchini Marekani mwaka huu pekee, kumefanyika mashambulizi 240 yanayolenga watu wengi huku baadhi ya wadadisi wakisema mauaji hayo mengi yanaashiria kuanza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Mauaji ya silaha moto na ufyatulianaji risasi wa kiholela umekuwa mkubwa nchini Marekani kiasi kwamba serikali na jeshi la polisi la nchi hiyo haliwezi tena kudhibiti uhalifu huo. Sasa hivi mauaji hayo yanatokea kila siku si mwishoni mwa wiki tu kama ilivyokuwa hapo kabla. Joe Biden amekiri kushindwa kudhibiti uhalifu huo na kulitupia kazi hiyo Baraza la Congress akilitaka lidhibiti kasi ya kiwango cha juu ya matumizi ya holela ya silaha moto nchini Marekani