Idara ya Ulinzi ya Uingereza: Waukraine wabomoa madaraja baada ya kurejea nyuma

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, imeeleza kua kilomita 90 ya mstari wa mbele wa vita kati ya vikosi vya Kirusi na Kiukreni ziko magharibi mwa Mto Siversky Donetsk na kusema kua kuvuka kwa Warusi kwenye mto huu ni uamuzi bora na muhimu.

Baada ya kukiri kuwa jeshi la Ukraine lilikuwa limejiondoa kutoka mstari wa mbele wa vita na Urusi katika eneo la Sverodontsk, London wakati huu ilitangaza juhudi za vikosi vya Urusi kuvuka mto muhimu kistratejia, uliopo mashariki mwa Ukraine.

Mkuu wa harakati ya ujasusi wa jeshi la Uingereza alisema Jumatatu kwamba mapigano karibu na Siurodonsk yaliongezeka mwishoni mwa juma.

Kuvuka kwa mto huo kuna uwezekano kuwa mojawapo ya viambatisho muhimu vya vita ndani ya miezi ijayo.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza iliendelea kwa kusema: “Urusi lazima ichukue hatua mbadala au ishambulie vivuko vya mito ili iweze kufanikiwa katika awamu ya sasa ya operesheni na kuivamia Dunbas.”

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov amesema takriban ndege 1,500 za kijeshi za Ukraine, zikiwemo ndege za kivita, helikopta na UAV na takriban vifaru 3,500 na mifumo 500 ya makombora, zimeharibiwa tangu kuanza kwa operesheni ya kivita katika eneo la Donbas.

 

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *