Saudi Arabia yaondoa sharti la kuvaa barakoa ndani ya msikiti mtukufu wa makka

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia iliondoa sharti la matumizi ya barakoa katika maeneo yenye msongamano wa wtu wengi isipokua ndani ya Masjid al-Haram na Masjid al-Nabi.

Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia ‘Wass’ limemnukuu afisa mmoja katika Wizara ya Mambo ya Ndani akisema kuwa vikwazo vingine vya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo vitaondolewa kutokana na ufuatiliaji wa maradhi ya moyo na matokeo mazuri yatakayopatikana.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, sharti la kutumia barakoa lilifutwa katika sehemu kadhaa isipokua ndani ya Masjid al-Haram na Masjid al-Nabi s.a.w.w na maeneo mengine ambapo maagizo maalum ya kiafya yalitolewa katika sehemu zinazohitaji kiwango cha juu cha kinga.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imeongeza muda wa kupokea dozi ya tatu ya chanjo ya Corona kwa raia wanaotarajia kusafiri nje ya nchi kutoka miezi mitatu hadi miezi minane baada ya kupokea dozi ya pili.

Mnamo mwezi Aprili, wizara ya Hija na Umra ya Saudi Arabia ilitangaza katika taarifa yake kwamba imeamua kuongeza idadi ya mahujaji kutoka ndani na nje ya Saudi Arabia (wakati wa maadhimish ya Hijatu Tamatu’) hadi milioni moja.

Wizara hiyo pia iliongeza kuwa Hija ya mwaka huu (hijatu tamatu’) itakuwa ya mahujaji walio na umri wa chini ya miaka 65, na kwamba lazima wawe wamepokea dozi za kimsingi za chanjo ya corona ziliyoidhinishwa na Wizara ya Afya ya Saudia.

Wizara ya Hija na Umra ya Saudia imesisitiza haja ya mahujaji kuzingatia hatua na masharti yaliowekwa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona na kudumisha afya zao wakati wa ibada za Hija.

Miaka miwili iliyopita, Saudi Arabia ililazimika kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya mahujaji wanaohudhuria ibada ya Hija kutokana na kuenea kwa virusi vya corona.

Idadi ya mahujaji kwenye ibada ya Hajj tamatu’ kabla ya ugonjwa wa corona mwaka 2019 ilikuwa takriban milioni 2.5, lakini kutokana na kuenea kwa virusi mnamo mwaka 2020, Saudi Arabia iliruhusu watu 1,000 pekee kushiriki kwenye hijja ya Tamatu’. katika mwaka uliofuta Idadi hii iliongezeka na kufikia 60,000 ambayo kwa kupitia zoezi la kura walichaguliwa wale walipiga dozi ya chanjo.

 

 

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *