Jenerali mmoja wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ameashiria udhaifu wa jeshi la utawala huo na kusisitiza kuwa, endapo hali hiyo haitabadilika, Israel haitashinda katika vita vijavyo.
Kwa mujibu wa chaneli ya 14 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni, Yitzhak Barik, jenerali mkongwe katika jeshi la utawala haramu wa Israel na mkuu wa zamani wa kamati ya kuchunguza malalamiko ya wanajeshi, amekosoa hali ya vituo na kambi za jeshi la utawala wa Kizayuni na kusema: mwenendo na utendaji wa wanajeshi wa Israel hauendani na majukumu waliyonayo na wanazembea juu ya suala hilo.
Barik amesema, hivi karibuni alitembelea divisheni za jeshi la Israel na akafafanua kwamba, katika ziara yake hiyo ameshuhudia waziwazi jinsi askari walivyopoteza ari na matumaini na wasivyoipa umuhimu nidhamu ya jeshi na akaongezea kwa kusema, ikiwa hali hiyo haitaboreshwa, jeshi la Israel halitapiga hatua na halitaweza kupata ushindi katika vita vyovyote vya siku za usoni. Hivi karibuni pia Jenerali Yitzhak Barik alitahadharisha kwamba ikiwa utawala wa Kizayuni utaingia katika vyovyote siku za usoni, wanajeshi wengi wa utawala huo haramu watauawa.
Hivi sasa miaka 74 imepita tangu ulipoundwa utawala haramu na ghasibu wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu. Kama huko nyuma, utawala wa Kizayuni ulikuwa ukikabiliana zaidi na changamoto za nje, hivi sasa unashuhudia mchanganyiko wa changamoto za ndani na nje; na kwa mtazamo wa shakhsia na viongozi wa utawala huo, changamoto za ndani ni kubwa na nyingi zaidi. Ni kutokana na hali hiyo waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Naftal Bennett amesema ana wasiwasi juu ya mustakabali wa Israel na kutahadharisha juu ya kushtadi matokeo hasi ya changamoto zinaoukabili utawala huo.