Afrika Kusini yataka utawala wa Kizayuni wa Israel uadhibiwe kimataifa

FARAAN: “Arabi 21” imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mwito huo umetolewa Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Bi Naledi Pandor kwenye kikao cha Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki Zisizopingika za Taifa la Palestina na kuitaka jamii ya kimataifa kumaliza mateso ya Wapalestina kwa kuuadhibu kimataifa utawala wa Kizayuni.

Afrika Kusini imesema kwenye kikao hicho kwamba wananchi wa Palestina wako chini ya mateso makubwa ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa miaka 73 sasa na kwamba kila mwenye hisia za kibinadamu anataka mateso hayo yakomeshwe mara moja. Jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Palestina zinaendelea bali kila siku zinazidi kuwa kubwa na wazi zaidi.

Bi Pandor aidha amesema: “Sisi wananchi wa Afrika Kusini, wakati tunapoona hali mbaya ya Wapalestina, tunakumbuka hali yetu mbaya tuliyokuwa nayo (wakati wa utawala wa makaburu). Vile vile tunakumbuka wakati wa maziko ya Shireen Abu Akleh na jinsi wanajeshi wa Israel walivyoshindwa kuvumilia hata kuona jeneza tu la mwandishi huyo (aliyepigwa risasi na kuuliwa kidhulma na wanajeshi hao Wazayuni).”

Taarifa za karibuni kabisa kutoka Palestina zinasema kuwa, jeshi katili la utawala haramu wa Israel limewaua shahidi vijana watatu wa Kipalestina katika mji wa Jenin wa kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Wafa ambalo limeeleza kuwa, vijana hao wa Kipalestina waliuliwa shahidi alfajiri ya jana Ijumaa baada ya wanajeshi makatili wa Israel kushambulia kambi hiyo ya wakimbizi ya Jenin.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *