Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) alikutana na rais wa Lebanon katika Ikulu ya Baabda.
Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Ismail Haniya, amekutana leo (Ijumaa) na Rais wa Lebanon Michel Aoun.
Haniya alisema baada ya mkutano huo ” alisisitiza kuwa utawala haramu unaoukalia kwa mabavu aridhi ya Palestina hautofautishi kati ya Waislamu na Wakristo wa Palestina, hasa huko katika mji wa Jerusalem,”
Haniya alinukuliwa na Al-Manar akisema “Tulielezea pia mshikamano wetu na rais wa Lebanon na upinzani wake dhidi ya wizi wa utajiri wa nchi yake wa baharini unaofanywa na adui na utawala haramu wa Israel, na tunatumai kuwa Lebanon itafikia usalama zaidi, utulivu na umoja.
Ismail Haniya, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, aliwasili Lebanon Jumanne iliyopita akiongoza ujumbe wa ngazi za juu.
Siku ya Jumatano, Haniya pia alikutana na Mufti Mkuu wa Lebanon, Sheikh Abdul Latif Daryan. Katika kikao hicho, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amepongeza nafasi na misimamo ya Mufti wa Bahari kuhusu Quds, anavyolitetea ndani na nje ya nchi.
Siku ya Alkhamisi, idara ya uhusiano wa umma ya Hizbullah ya Lebanon ilitangaza katika taarifa yake kuwa Ismail Haniya na Sayyid Hassan Nasrullah wamekutana na kubainisha kuwa pande hizo mbili zimejadili kuhusu maendeleo ya kisiasa huko Palestina, Lebanon na eneo zima kwa ujumla.