Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kiislamu nchini Uingereza (IHRC) amesema kuwa mfumo wa utawala wa Marekani unapinga na kupiga vita haki za binadamu na kusisitiza kuwa, mfumo huo unawadhulumu hata raia wa Marekani kwenyewe.
Massoud Shajareh amesema inasikitisha kuona kwamba Marekakni imezifanya haki za binadamu kuwa fimbo na kutangaza kuwa, Washington inatumia haki za binadamu kwa ajili ya kukidhi maslahi yake na haichungi viwango vya haki hizo.
Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kiislamu nchini Uingereza amesisitiza kuwa, tunapozungumzia upinzani dhidi ya Marekani, hatuna maana ya kuwapinga wananchi wa nchi hiyo, bali ni kupinga mfumo wa serikali ya Washington ulio dhidi ya haki za binadamu. Massoud Shajareh amesema, mkono wa serikali ya Marekani unaonekana katika mauaji yote yanayotokeo katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Amesema Wamarekani wameua wenyeji milioni 15 katika kipindi cha miaka kadhaa, na kuongeza kuwa: “Asilimia moja tu ya watu wa Marekani wanamiliki asilimia 89 ya rasilimali za kifedha na madaraka, na asilimia 99 ya Wamarekani wanakandamizwa na kunyanyaswa.
Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza pia amesema kuwa, inasikitisha kwamba, katika kipindi chote cha historia wakoloni wameweza kuficha jinai na uhalifu wao kupitia vyombo vyao vya habari, na kwamba Marekani inafanya hivyo hivyo.